Mwanamfalme wa
Jordan Ali Bin Al-Hussain ametangaza kuwa atasimama kuwania nafasi ya
Urasi wa Shirikisho la kandanda duniani FIFA kurithi nafasi ya Rais wa
sasa anayestaafu Sepp Blatter.
Wakati wa uzinduzi wa kampeni zake
mwanamfalme huyo aliahidi kufanya mageuzi katika uongozi wa
soka,kupambana na rushwa na kuimarisha soka la wanawake.Alipoteza
ushindi mwezi Mei ambapo Sepp Blatter alishinda kabla ya kutangaza
kujiuzulu wadhifa huo.Maafisa wa ngazi ya juu ya FIFA wanatuhumiwa kuhusika na rushwa na mamlaka za Marekani mapema mwaka huu.
Rais wa shirikiso la soka barani Ulaya Uefa Michel Platini na Chung Mong-joon wa Korea Kusini kwa pamoja wameonesha nia yao kuwania nafasi hiyo ambao uchaguzi wake utakua mwezi Februari mwaka 2016.
No comments:
Post a Comment