Tuesday, September 1, 2015
Habari za mpya za usajili Ulaya
Hivi sasa ni kwamba Emanuel Adebayor yupo kwenye maongezi na West Ham ili kukubaliana matakwa yake binafsi na kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kutoka Spurs.
Hivi sasa maongezi yanaendelea kati ya Cavani na Arsenal huko Paris na habari zinaweza kutoka ndani ya muda wowote kuanzia sasa hivi. Arsene Wenger anaripotiwa kuwa huko kwa ajili ya kikao hicho.
Everton wame-conferm kumsajili beki Ramiro Funes Mori kwa gharama ya £9.5m. Mkataba wake ni wa miaka 5.
Kuhusu David De Gea na habari zinazokwamisha uhamisho wake kukamilika kuna document zinahitajika ili kukamilisha dili hilo. Karatasi hizo ni kama Player’s identity, Player’s employment details, Agreed transfer fees na Intermediary involvement.
Southampton wamesema kwamba wanakaribia kukamilisha usajili wa Virgil Van Dijk na Wanyama, Sadio Mane hawaondoki kwenye hiyo club.
Alex Song ambae amejiunga na West Ham amepiga picha wakiwa kwenye furaha na Adebayor na inasemekana kwamba amemshawishi Adebayor kujiunga na West Ham.
Foward wa Manchester United Joe Bernstein mwenye miaka 21 inasemekana kwamba anaweza kujiunga na Spurs au WestBrom ambao wapo kwenye harakati za kutumia muda mfupi uliobaki ili kumsajili.
Davis Gold ndie aliyetoa conformition kuhusu Alex Song kusaini mkataba wa mkopo wa muda mrefu na Wrst Ham. Ikumbukwe aliwai kucheza West Ham.
Endelea kufuatilia Live updates hapahapa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment