Kuna
tabia fulani ambazo humfanya Vincent Kompany kuwa moja ya mabeki wenye
mioyo iliyojaa hali ya ushindani muda wote katika ligi kuu nchini
Uingereza.
Mbelgiji huyo si tu kana kwamba
yuko ngangari kwa muonekano bali tu, bali pia ni mkatili na mshindani
pindi awapo uwanjani. Amezaliwa na chembechembe za ushindi ndani ya moyo
wake ambapo wakati wote anaweza kufanya chochote ili mradi tu timu yake
ipate matokeo.
Kwa nini yanasemwa maneno hayo,
ni kutokana na kile alichokifanya kwa binti yake mwenye umri wa miaka
mitano (5) anayejulikana kwa jina la Sienna. Kompany alionekana
akimkimbiza mwanae na wakati alipotaka kujifanya mjanja wa kukimbia,
alimkwatua kidogo na kumuangusha chini bila ya kumletea maumivu yoyote
yale.
No comments:
Post a Comment