Tuesday, September 15, 2015

Ligi ya mabingwa Ulaya kutimua vumbi leo

 

 

Msimu mpya wa michuano ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya kwa msimu wa 2015-2016 utaanza leo kwa nyasi za Viwanja vinane kuwaka moto.
Katika kundi A, PSG itawaalika timu ya Malmo Ff kutoka Sweden huku Real Madrid, wakiwa wenyeji wa Shakhtar Donetsk, mchezo utakaopigwa kwenye Dimba la Santiago Bernabéu.
Katika kundi B PSV Eindhoven, ya Uholanzi watakua wenyeji wa Manchester United, toka Uingereza huku mchezaji wa zamani kwa kikosi hicho Memphis Depay, akirejea kucheza na timu yake hiyo ya zamani. Mchezo wingine wa kundi hili VfL Wolfsburg, ya Ujerumani watashuka dimbani kuwakabili CSKA Moscow, kutoka Urusi.
Michezo mingine itayopigwa leo hi ya michuano hii.
Kundi C
Galatasaray na Atletico Madrid
Benfica na FC Astana
KUNDI D
Man City na Juventus
Sevilla na Borussia Monchengladbach

No comments:

Post a Comment