Kocha
mstaafu wa Manchester United Sir Alex Ferguson katika kitabu chake
kipya cha hivi sasa, amewataja wachezaji wanne wa kiwango cha dunia
kuwahi kuwafundisha.
Alex Ferguson amemtaja Cristiano
Ronaldo kuwa ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kumfundisha huku
akiwaongeza Erick Cantona, Ryan Giggs na Paul Scholes kama wachezaji
wake bora wa kiwango cha dunia.
Alex
anasema, “katika kitabu changu kuna wachezaji wawili tu wa kiwango cha
dunia ambao bado wanacheza hadi sasa, Ronaldo na Messi”.
Katika orodha hiyo hakuna majina ya wachezaji Wayne Rooney, David Beckham wala Rio Ferdinand.
Lakini Fergie anasema aliowataja,
wamethibitisha ubora wao huku akimwagia sifa Ryan Giggs kwamba atakuja
kuwa ni kocha mkubwa na mafanikio mengi siku moja.
Akiongea kuhusu kitu
anachokijutia katika maisha yake ya ukocha, Fergie anasema ni
kutokushinda mataji mengi ya Ulaya ingawa alishinda makombe mbalimbali
ya nyumbani.
No comments:
Post a Comment