Saturday, September 26, 2015

Pele ataja timu ambayo angecheza England

Pele

Nguli wa soka ulimwenguni, Pele amesema kama angepata fursa ya kucheza ligi kuu nchini Uingereza, basi angekipiga kunako klabu ya Arsenal.
Pele amedai kuwa mtindo wanaocheza Barcelona unafafana sana timu yake ya zamani ya Santos, ambayo aliichezea kati ya mwaka 1956 na 1974.
Alipoulizwa ni timu gani angependa kucheza nchini Uingereza, Pele alijibu.
“Arsenal ingekuwa ndio sehemu pekee ambayo ningeweza kucheza”,  Pele aliliambia gazeti la Telegraph .
“Napenda sana timu ambazo hucheza mchezo wa kujiachia/kufunguka uwanjani. Kwa sasa ni vigumu mno kusema ni timu gani ambayo inacheza mchezo huo.
Bosi: Pele angejikuta kwa sasa akiwa chini ya Arsene Wenger
Pele anasema staili ya Barcelona inakaribiana na ile ya timu yake ya zamani ya Santos”.
“Kati ya Chelsea na Arsenal? Ningependa kucheza Arsenal kama ningepata hiyo fursa”.

No comments:

Post a Comment