Kamati maalum ya
kutoa msamaha imeanza kukutana mjini Durban Afrika Kusini kutathmini
iwapo mwanariadha Oscar Pistorius anastahili msamaha na kuwachiliwa huru
au la .
Vikao hivyo katika mji wa Durban vinatarajiwa kubaini
iwapo Pistorius aliyehukukumiwa kifungo cha miaka 5 gerezani
atawachiliwa huru ama aendelee kutumikia kifungo cha miaka 5 jela. Waziri wa haki nchini humo, alizuia mwanariadha huyo kuachiliwa huru mwezi uliopita kama ilivyokuwa imetarajiwa.
Waziri huyo alisema kuwa uamuzi wa kamati hiyo ya kutoa msamaha wa kumuachilia mwanariadha huyo, baada ya kutumikia kifungo cha miezi kumi ya kifungo chake cha miaka mitano ulitolewa mapema na kuwa haukuwa na msingi wowote kisheria.
Mahakama nchini humo ilimpata Pistorius na hatia ya kuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka wa 2013.
Pistorius alimpigia risasi Steenkamp akiwa bafuni nyumbani kwake mjini Pretoria, baada ya kumshuku kuwa ni mwizi.
Upande wa mashtaka umekataa rufaa ya hukumu hiyo ukisema kuwa Pistorius anapaswa kuhukumiwa kwa mauaji.
Chini ya sheria za Afrika Kusini,mtu anaweza kusamehewa mradi ametumikia sehemu moja juu ya 6 ya kifungo chake gerezani na awe na nidhamu njema.
Mawakili wa Pistorius wanatarajiwa kuwasilisha nyaraka zao kupinga rufaa hiyo.
No comments:
Post a Comment