Thursday, September 17, 2015

Matokeo yote ya Ligi Kuu Tanzania bara ya jana


VPL logo
Mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara zimeendelea jana kwenye viwanja saba huku timu 14 zikipambana viwanjani kuwania pointi tatu muhimu kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi hiyo msimu huu.
Jijini Tanga wenyeji Mgambo JKT walikuwa wakiwaalika ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba kwenye uwanja wa Mkwakwani ambapo Simba wamechomoza na ushindi wa goli 2-0 magoli yaliyofungwa na Justice Majabvi na Hamisi Kiiza.
Timu ya Majimaji ikiwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea imechomoza na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Kagera Sugar, pambano jingine lilikuwa ni kati ya Toto Africans ‘wana kishamapanda’ ambao wao walikuwa nyumbani kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Mtibwa Sugar mchezo uliomalizika kwa Mtibwa kutwaa pointi tatu kwa kuifunga Toto goli 2-0.
Kwenye dimba la Sokoine, timu ya Mbeya City imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya maafande wa JKT Ruvu. Azam wakiwa ugenini kwenye uwanja wa CCM Kambarage wamefanikiwa kuitungua Stand United kwa goli 2-0 wakati Ndanda FC wakiwa nyumbani kwenye dimba la Nangwanda Sijaona wameandika ushindi wa kwanza wakiichapa Coastal Union kwa goli 1-0.

No comments:

Post a Comment