Thursday, September 10, 2015

Twiga Stars yatupwa nje michezo ya Afrika

TIMU ya Nigeria ‘Super Falcons’ imeifunga Tanzania mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi A Michezo ya Afrika inayoendelea Kongo Brazzaville.
Kipigo hicho cha Nigeria Inayofundishwa Christopher Musa Danjuma kinakuwa cha pili kwa Tanzania, baada ya awali kufungwa 1-0 na Ivory Coast katika mchezo wa kwanza hivyo kuishia hatua ya makundi.
Aidha, hii inakuwa mara ya pili Nigeria inaichapa Tanzania 3-0, baada ya mwaka 2010 kuifunga hivyo hivyo pia kwenye MIchezo hiyo hiyo ya Afrika. 
 
Super Falcons sasa inajihakikishia kwenda Nusu Fainali za michuano hiyo kwa pointi zake sita baada ya kuwafunga wenyeji Kongo 5-1 katika mchezo wa kwanza.
Mchezo mwingine wa kundi hilo unafuatia hivi sasa kati ya Kongo na Ivory Coast. Nigeria itamaliza na Ivory Coast, wakati Tanzania itamaliza na Kongo kabla ya kurejea nyumbani.
Kikosi cha Nigeria kilikuwa; Oluehi Tochukwu, Edoho Blessing, Osinachi Marvis Ohale, Osarenoma Igbinovia, Onome Ebi, Gladys Akpa, Wogu Chioma Success, Ugochi Desire Oparanozie, Ukpong Esther Sunday, Adeboyejo Yetunde Oluwatosin na Nwabuoku Evelyn Chiedu.
Tanzania; Fatuma Omar Jawadu, Anastas Katunzi, Stumai Athumani, Amina Bilal, Fatuma Issa Maonyo, Donisia Minja, Mwanahamisi Shurua, Happyness Hezron, Fatuma Salum, Asha Rashid na Sophia Mwasikili.

No comments:

Post a Comment