Maandalizi ya mchezo kati ya
Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Nigeria (Super Eagles) yamekamilika,
ambapo leo Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza
viingilio vya mchezo huo wa jumamosi kati huku kiingilio cha chini
kabisa kikiwa shilingi elfu saba tu.
Viingilio vya mchezo huo wa
kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON Qaulifier 2017)
kundi G itakua ni VIP A Tsh 40,000, VIP B Tsh 30,000, VIP C Tsh15,000,
Rangi ya Machungwa (Orange) Tsh 10,000, na viti vya rangi ya Bluu na
Kijani Tsh 7,000.
Tiketi za mchezo huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa kesho siku ya ijumaa saa 4 kamili asubuhi katika vituo kumi vifuatavyo:
(i) Ofisi za TFF – Karume
(ii) Buguruni – Oilcom
(iii) Mbagala – Dar live
(iv) Ubungo – Oilcom
(v) Makumbusho – Stendi
(vi) Uwanja wa Taifa
(vii) Mwenge – Stendi
(viii) Kivukoni- Feri
(ix) Posta – Luther House
(x) Big Bon – Msimbazi Kariakooo
TFF inawaomba watanzania, wapenzi
na wadau wa mpira wa miguu kununua tiketi za mchezo huo katika magari
yaliyopo kwenye vituo vilivyotajwa ili kuondokana na tatizo la kuuziwa
tiketi zisizokuwa halali.
Jeshi la Polisi nchini kwa
kushirikiana na idara nyingine za kiusalama wameandaa usalama wa kutosha
katika kuelekea kwenye mchezo na kuhakikisha kila mpenzi wa mpira wa
miguu anaingia kushuhudia mchezo huo salama na kuondoka salama.
Mchezo huo utaanza saa 10:30
jioni kwa saa za Afrika Mashariki utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini
Rwanda ambao wanatarajiwa kuwasili leo jioni pamoja na kamisaa wa mchezo
huo.
Waamuzi wa mchezo huo ni Louis
Hakizimana (mwamuzi wa kati) Honore Simba (mwamuzi msaidizi), Jean Bosco
Niyitegeka (mwamuzi msaidizi), Abdoul Karim Twagiramukiza (mwamuzi wa
akiba) wote kutoka Rwanda na kamisaaa ni Charles Kasembe kutoka nchini
Uganda.
No comments:
Post a Comment