Huwezi
kutaja radha za kuangalia ligi kuu soka nchini Spain, La Liga bila
kufuatilia ushindani wa magwiji wa soka hivi sasa ulimwenguni Cristiano
Ronaldo na Lionel Messi.
Ushindani kati ya wawili hao
umeleta hisia tofauti na mvuto wa aina yake katika ligi hiyo na kuongeza
ladha ya pambano la El Classico ‘Real Madrid vs Fc Barcelona’ kutokana
na mashabiki kutaka kuona ni mchezaji yupi ataisaidia timu yake kuibuka
shujaa.
Hadi sasa zimechezwa mechi mbili
kwenye ligi hiyo kwa kila timu, lakini hakuna yeyote kati ya wawili hao
ambae tayari amefunga goli. Kitu hicho kimepelekea utani wa kusema kuna
uchawi unaendelea baina ya miamba hao ambao huwa na kawaida ya
kushindana kila mmoja akitaka kufunga zaidi ya mwenzake.
Ligi bado mbichi na wengi
wanaamini siku Messi akifunga goli na upande wa pili utajibu mapigo,
Ronaldo naye atafunga, tusubiri kuona hilo.
Wawili hao wamekua wakishindana
kwa kila hali, idadi ya magoli, hat-trick pamoja na tuzo binafsi kama za
Ulaya na dunia kwa ujumla kitu kilichoongeza utamu wa la liga katika
miaka sita hivi sasa.
No comments:
Post a Comment