Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) leo limesaini mkataba wa udhamini wa ligi daraja la
kwanza (FDL) na kampuni ya Star Times Media wenye thamani ya shilingi
milioni miatisa za kitanzania kwa muda wa miaka mitatu ili kusaidia
gharama za uendeshaji wa ligi hiyo.
Utiaji saini huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Kisenga Millennium Towers, Makumbusho kati ya TFF na Star Times.
Rais wa TFF Jamal Malinz
ameishukuru Star Times kwa kukubali kudhamini ligi hiyo ili kuzisaidia
timu shiriki kujikimu pamoja na bodi ya ligi kuwalipa waamuzi pamoja na
garama nyingine za uendeshaji wa ligi hiyo ambazo zimekuwa zikibebwa na
TFF kwa miaka yote.
Malinzi amesema, kila timu
itapata shilingi milioni 15. Milioni 10 kati ya hizo inatoka moja kwa
moja Star Times wakati milioni tano itatoka kwenye haki za matangazo ya
television kutokana na ligi hiyo kuonekana moja kwa moja (live) kupitia
ving’amuzi vya Star Times.
Hata hivyo Malinzi amefafanua
kuwa, mkata uliosainiwa leo ni wa udhamini wa ligi kutoka Star Times
lakini wiki ijayo watasaini mkataba mwingine na kampuni nyingine
itakayopewa haki ya kurusha matangazo ya mechi za ligi daraja la kwanza.
Liao Lan Fang ambaye ni
mkurugenzi mkuu wa Star Times amesema, mbali na udhamini huo wa shilingi
milioni miatisa, vilabu hivyo vitapta fursa ya kuonekana moja kwa moja
kwenye nchi zaidi ya 10 za Afrika ambapo Star Times inapatikana.
No comments:
Post a Comment