Saturday, September 19, 2015

Nyota wa zamani wa Yanga awika Afrika Kusini

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga SC, Mliberia Kpah Sherman jana ametokea benchi na kuisaidia timu yake mpya, Mpumalanga Black Aces kupata sare ya 1-1 na Orlando Pirates katika Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Orlando Pirates, wenyeji ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 21 kupitia kwa Mpho Makola kabla ya mkongwe wa Zambia, Collins Mbesuma kuwasawazishia Black Aces dakika ya 45.
Sherman aliyeondoka Yanga SC mwezi uliopita baada ya kuichezea kwa nusu msimu, aliingia dakika ya 81 kwenda kuchukua nafasi ya Mbesuma na akacheza vizuri na kukaribia kufunga mara mbili.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Sherman kucheza Pirates baada ya kupata kibali cha kufanya kazi Afrika Kusini. 
Kikosi cha Pirates kilikuwa; Ovono, Mahamutsa, Gyimah, Jele, Matlaba, Ntshumayelo/Majafa dk63, Maslaesa, Makola/Myeni dk34, Rkhale, Masuku/Erasmus dk77 na Majoro.
Black Aces; Walters, Kobola, Ngalo, Mzava, Nonyane, Manyama, Khuboni, Ngoma, Jayiya, Tukane/Modiba dk68 na Mbesuma/Sherman dk81.

No comments:

Post a Comment