Nyota
wa mchezo wa Tennis duniani Victoria Azarenka, amemimina pongezi kwa
mchezaji mwenye kipaji cha ajabu ulimwenguni Lionel Messi, huku
akisisitiza kwamba hucheza kama yupo kwenye ‘video game’ pindi awapo
uwanjani.
Messi aliifungia Argentina mabao
mawili katika ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Bolivia Jumamosi wiki ya
iliyopita, japokuwa bado hajafunga katika michezo miwili ya ufunguzi wa
La Liga kwa timu yake mpaka sasa.
Mbelarusi huyo mwenye umri wa
miaka 26, ambaye amefika robo fainali ya michuano ya US Open na kutoa
shukrani zake za dhati kwa mashabiki baada ya ushindi wake dhidi ya
Varvara Lepchenko, amesema kuwa uwezo wa nyota huyo wa Barcelona ni kitu
kama “kisichofikirika” na kuongeza kuwa mara nyingi humwangalia wakati
akiwa mapumzikoni.
“Kumwangalia Messi akicheza ni kama vile unaangalia video game”, aliwaambai waandishi. “Ni kitu cha kusisimua sana”.
“Nisingeweza kuangalia mchezo ule
kwa sababu ya tofauti ya masaa na kwa sababu siku hizi nina majukumu
mengi kidogo, lakini ningeweza kumwangalia kwa sababu ya umaridadi
wake”.
“Anachokifanya Messi uwanjani ni
kitu kisichoelezeka. Huwa najisikia furaha kubwa sana ninapomuangalia
hasa akiwa na Barcelona na kusema tu ukweli, kwangu mimi, jamaa ni wa
ajabu sana”.
Azarenka alimalizia kwa kusema:
“Wacheza soka hucheza kwa kutumia miguu. Siwezi kusema kwamba sidhani
kama ubora wa mikono yangu katika Tennis ni kama yeye katika soka,
lakini najaribu”.
No comments:
Post a Comment