Arsenal inaanza
kampeni yake katika michuano ya vilabu bingwa Ulaya siku ya jumatano
ikiwa itakabiliana na Dinamo Zagreb katika uwanja wa Stadio Maksimir.
Mkufunzi
Arsene Wenger amekuwa akikosolewa kwa kushindwa kununua mshambuliaji
mpya, lakini anasema kuwa anakiamini kikosi chake na kwamba Theo Walcott
ndio jibu la safu yake ya mashambulizi.Pia amesema kuwa ni muhimu kwa kikosi chake kutoshindwa katika mechi ya kwanza ya michuano hiyo nchini Croatia.
No comments:
Post a Comment