Saturday, September 19, 2015

Carlos: Neymar ni bora zaidi kuliko Ronaldo, Messi

neya
Kila siku story inayoleta mdahalo ni kujaribu kujua nani mchezaji mkali kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi. Jibu bado halijapatikana ukizingatia Messi kamaliza vizuri msimu uliopita na Cristiano Ronaldo anaelekea kufanya hivyo hivyo msimu huu kwa kasi aliyoanza nayo.
Sasa Roberto Carlos mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil alivyoulizwa swali maarufu sana kuhusu nani mkali kati ya Ronaldo na Messi alisema hivi,“Watu kila siku wanamzungumzia wale wale Messi na Ronaldo lakini ningependa kumzungumzia Neymar. Kwa upande wangu Neymar ni mkali zaidi yao”
“Hao wengine ni wakali pia lakini mimi namchagua Neymar, ukimuangalia Cristiano Ronaldo ni mchezaji ambae anajitengeneza mwenyewe, ana nidhamu ya kazi na anachokifanya kinavutia hivyo hivyo kwa Messi kazi anayofanya ni kubwa hadi anashinda Ballon d’Or.”

No comments:

Post a Comment