Thursday, September 17, 2015
Shabiki namba moja wa Brazil afariki dunia akiwa na miaka 60
Kama wewe umeanza kushabikia soka siku hizi za karibuni basi karibu kwenye ulimwengu wa soka, lakini kama wewe ni mkongwe basi kuna mkongwe mwenzako anaitwa Clovis Acosta Fernandes amefariki dunia.
Shabiki huyu maarufu wa timu ya taifa ya Brazil ambae alipewa jina la mchezaji wa 12 wa Brazil amefariki akiwa na miaka 60. Huyu jamaa sura yake ilikua kwenye TV za michuano ya kombe la dunia tangu 1990. Kuanzia kipindi hicho Brazil inatesa hadi mechi ya Brazil inafungwa 7-1 huyu jamaa alikua uwanjani na hajawai kukosa hata mara moja michuano ya kombe la dunia.
Chanzo cha kifo cha huyu jamaa ni kansa ambayo alikua anapambana nayo kwa muda miaka 9 lakini mwaka huu ndio imemchukua.
Hadi FIFA wametumia page zao za mitandao ya kijamii kuonyesha masikitiko yao juu ya kifo cha huyu jamaa ambae alikua ni zaidi ya shabiki wa michuano ya kombe la dunia. Rest in Paradise Fellow Football Fanatic
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment