Wednesday, September 2, 2015

Mwaikimbia aifunga timu yake ya zamani




 
 
 
 
 
 
 
 
MSHAMBULIAJI Gaudence Mwaikimba usiku wa kuamkia leo ameiadhibu timu yake ya zamani, Azam FC akitoa mchango mkubwa kwa timu yake mpya, JKT Ruvu kushinda mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, ambao kocha Muingereza Stewart Hall aliwakosa nyota wake wa kikosi cha kwanza walio na timu za taifa, JKT Ruvu walipata bao la kwanza dakika ya 10 Mwaikimba akimalizia shuti la Mussa Said akitumia makosa ya kipa Mwadini Ali.
Hata hivyo, bao hilo halikudumu sana, kwani Azam FC walisawazisha kupitia kwa Kipre Herman Tchetche dakika tano baadaye, akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya JKT.
JKT Ruvu inayofundishwa na beki wa zamani wa Yanga SC, Freddy Felix Minziro ilipata bao lake la ushindi dakika ya 85 mfungaji Najim Magulu aliyemalizia pasi ya Mwaikimba baada ya beki Bryson Raphael kuchanganyana na kipa wake Mwadini Ali.
Mchezo huo ulikuwa maalum kwa timu zote kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza wiki ijayo.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Serge Pascal Wawa, Gardiel Michael, Lacine Diouf/Said Mourad dk47, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Bryson Raphael, Ame Ally, Kipre Tchetche na Ramadhani Singano ‘Messi’/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk60. 
JKT Ruvu: Tony Kavishe, Napho Zubery, Edward Charles, Cecil Kisimba, Martine Kavila, Hamisi Shengo, Ismail Mohammed/Emanuel Pius dk20, Matheo Daniel/Issa Ngao dk80, Gaudence Mwaikimba, Amour Janja/Najim Magulu dk76 na Mussa Said/Jaffar Kisoky dk80.

No comments:

Post a Comment