Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji
wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo
iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia
mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa
kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000)
kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John
Bocco.
Nyoso alifanya kitendo hicho
katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City
uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa
tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye
michezo ya Ligi Kuu.
Klabu ya Young Africans imepigwa
faini ya shiligi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake watano
kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa
kanuni namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake watapata kadi zaidi ya
tano katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano.
Wachezaji waliopata kadi za njano
wa Young Africans katika mchezo huo ni Salum Telela, Mbuyu Twite,
Malimi Busungu, Ali Mustafa na Mbuyu Twite.
Aidha klabu ya Yanga imepigwa
faini nyingine ya shilingi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake
kwenda kushangilia upande wa Simba SC mara baada ya mchezo kumalizika.
Mchezo utatazamwa tena ili kuangalia malalamiko ya Simba SC dhidi ya mwamuzi.
Simba pia inapigwa faini baada ya
wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwashambulia waamuzi baada ya mchezo
ambapo waliwarushia chupa za maji ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na
kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.
Mchezo namba 26 wa VPL kati ya
Coastal Union na Mwadui uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Chumba cha Coastal Union kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya
mashabiki wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli la upande wa
kaskazini walitoa lugha ya matusi kwa waamuzi na kutishia kuwapiga na
pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii Mohamed na jiwe
moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba msaada wa
jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika 3.
Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti wa wachezaji Coastal Union itatozwa faini ya Tsh 500,000/=
Mchezo namba 22 wa VPL kati ya
Mtibwa Sugar na Ndanda uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu, Turiani.
Ndanda hawakuleta watu wa kutosha kwenye pre match meeting hivyo
wanapigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000/=)
Mchezo namba 23 wa VPL kati ya
Simba SC na Kagera Sugar uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es
salaam. Simba walikuwa na wajumbe watatu na Kagera Sugar walikuwa na mtu
mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote zimepigwa faini ya shilingi
laki mbili (200,000).
Mchezo namba 17 wa VPL kati ya
Stand united na African Sports kocha wa Stand United alitolewa nje ya
eneo la ufundi kwa kutoheshimu taratibu za eneo hilo na pia alikataa
kuongea na vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu wa kanuni namba 40 (11)
anafungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mechi mbili na faini ya sh
500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.
Friends Rangers na KMC Mechi Na 8
Kundi A iliyofanyika uwanja wa Karume 27.9.2015. Timu ya KMC ya
Kinondoni ilifanya mabadiliko kwa kuingiza wachezaji 4 ambao ni kinyume
cha kanuni. Kwa mujibu wa taarifa ya mwamuzi wachezaji waliofanyiwa
mabadiliko ni
i. Frank Mashoto badala ya Kudra Omari
ii. Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon
iii. Mfanyeje Musa badala ya Kabange Mgunda na
iv. Sultani Kasiras badala ya Adam Said
Kwa mujibu wa kanuni namba 14
(25) KMC imepoteza mechi na kupigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa
akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati anapewa
onyo.
No comments:
Post a Comment