Saturday, September 19, 2015

Liverppol yaanza kwa sare Ligi ya Europa


MATOKEO MECHI ZA JANA UEFA EUROPA LEAGUE 
Asteras Tripolis 1 - 1 Sparta Prague 
APOEL Nicosia 0 - 3 FC Schalke 04 
Dnipro Dnipropetrovsk 1 - 1 Lazio 
Sporting Lisbon 1 - 3 Lokomotiv Moscow 
Skenderbeu Korce 0 - 1 Besiktas
Fiorentina  1 - 2 FC Basel
Tottenham Hotspur 3 - 1 FK Qarabag
Athletic Club 3 - 1 FC Augsburg
Lech Poznan 0 - 0 Belenenses
Partizan Belgrade 3 - 2 AZ
Ajax 2 - 2 Celtic
Viktoria Plzen 2 - 0 Dinamo Minsk
Napoli 5 - 0 Club Brugge
Bordeaux  1 - 1 Liverpool
FK Qabala 0 - 0 PAOK Salonika
FC Sion 2 - 1 Rubin Kazan
Slovan Liberec  0 - 1 Sporting Braga
SK Rapid Wien 2 - 1 Villarreal
Borussia Dortmund 2 - 1 FK Krasnodar
FC Groningen 0 - 3 Marseille
Fenerbahce 1 - 3 Molde
FC Midtjylland 1 - 0  Legia Warsaw
Kiungo wa Liverpool, Adam Lallana (kushoto) akipambana na Nicolas Maurice-Belay wa Bordeaux (kulia) katika mchezo wa Europa League jana

LIVERPOOL wamelazimisha sare ya 1-1 na Bordeaux ugenini katika mchezo wa Kundi B UEFA Europa League usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Matmut Atlantique, Ufaransa.
Adam Lallana alianza kuifungia Liverpool mjini Bordeaux dakika ya 65, kabla ya Jussie Ferreira Vieira kusawazishia wenyeji dakika ya 81.
Timu nyingine ya England, Tottenham Hotspur imeanza vyema kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya FK Qarabag mchezo wa Kundi J Uwanja wa White Hart Lane, London, mabao yake yakifungwa na Heung-Min Son dakika ya 28 na 30 na Erik Lamela dakika ya 86, huku wageni wakipata bao lao kwa penalti dakika ya saba kupitia kwa Richard Almeida.Fenerbahce striker Robin Van Persie was unable to add to his single goal since joining from United
Mshambuliaji wa Fenerbahce, Robin Van Persie alishindwa kufunga jana 

Mchezo mwingine wa kundi hilo, RSC Anderlecht imetoa sare ya 1-1 na Monaco bao likifungwa Guillaume Gillet dakika ya 11, kabla ya Lacina Traore kusawazisha dakika ya 85 Uwanja wa Constant Vanden Stockstadion.
Kundi K, FC Schalke ya Ujerumani imeshinda 3-0 ugenini dhidi ya APOEL Nicosia Uwanja wa GSP nchini Cyprus mabao ya Joel Matip dakika ya 28 na Klaas-Jan Huntelaar dakika ya 35 na 71.
Lazio imelazimisha sare ya 1-1 ugenini na Dnipro Dnipropetrovsk  katika mchezo wa Kundi G, bao lao likifungwa na Sergej Milinkovic-Savic dakika ya 34 kabla ya wenyeji kusawazisha dakika ya 90 na ushei kupitia kwa Evgen Seleznyov Uwanja wa Dnipro Arena.
Monaco 
Fiorentina imechapwa 2-1 katika mchezo wa Kundi I na FC Basel licha ya kuongoza kwa 1-0 hadi mapumziko kwa bao la Nikola Kalinic dakika ya tatu, kwani kipindi cha pili Birkir Bjarnason aliwasawazishia ugenini ya 71 na Mohamed Elneny akafunga la ushindi dakika ya 79 Uwanja wa Artemio Franchi.
Tottenham head coach Mauricio Pochettino opted to ring the changes for his side's Europa League opener with Qarabag 
Kikosi cha Tottenham kilichoiadhibu Qarabag jana 

No comments:

Post a Comment