Wednesday, September 30, 2015

Zlatan Ibrahimovic adhihirisha ni mchezaji wa namna gani

psg
Zlatan Ibrahimovic ikifika November 25 atakua na mechi dhidi ya Malmo. Club hii ambayo ina makazi nchini Sweden ndio sehemu ambayo Zlatan amezaliwa na kuanza kucheza soka, kwa hiyo Zlatan atakua anarudi nyumbani kwao asili yake kabisa.
Zlatan haioni hiyo mechi kama sehemu ya mashindano lakini kwake ni sehemu ya furaha kwake kurudi nyumbani. Mechi hii itakua kwenye group A la Uefa Champions League. group hilo lina club kama Paris,Real Madrid,Shakhtar Donetsk na Malmo.
Hivi sasa Zlatan ameshakodi eneo kubwa la wazi ambalo lipo kwenye maeneo hayo ya Malmo na ataweka big screen na hakuna mtu atakae lipia kiingilio kuangalia mechi hiyo. Zlatan ametoa tangazo hilo kwenye ukurasa wake wa instagram na kusema kwamba kuna suprise nyingi zinakuja.

Timu Ligi daraja la kwanza yabadilisha wachezaji wanne mechi moja

Friends Rangers 1 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, kumeshuhudiwa tukio la kushangaza kwenye soka la Tanzania baada ya timu ya KMC ya Kinondoni  inayoshiriki ligi daraja la kwanza (FDL) kufanya mabadiliko kwa kuwaingiza wachezaji wanne kitu ambacho ni kinyume cha utaratibu wa soka.
Tukio hilo lilitokea tarehe 27.9.2015 wakati KMC ikicheza dhidi ya Friends Rangers kwenye uwanja wa Karume ambapo KMC ilifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Frank Mashoto badala ya Kudra Omari, Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon, Mfanyeje Musa badala ya Kabange Mgunda na Sultani Kasiras badala ya Adam Said.
Mechi hiyo namba 8 ya Kundi A ilimalizika kwa KMC kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Friends Rangers.
Baadae Friend Rangers ilikata rufaa juu ya ushindi huo wa KMC kwasababu walikiuka kanuni na 14 (25) na maamuzi yaliyotolewa na TFF tarehe 30.9.2015 yameipa ushindi timu ya Friend Rangers huku KMC ikipigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati anapewa onyo.
IMG-20150929-WA0002
IMG-20150929-WA0001

Mwamuzi Nkongo kuchunguzwa kwa kuibeba yanga

 
KAMATI ya Uendeshaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imesema itautazama tena mchezo wa ligi hiyo kati ya Simba SC na Yanga SC uliofanyika Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ili ili kutathmini uchezeshaji wa refa, Israle Mujuni Nkongo.
Hiyo inafuatia malalamiko ya Simba SC iliyofungwa 2-0 kwamba Nkongo aliwaonea katika uchezaji wake, kiasi cha kufikiwa hadi kuwatukana wachezaji wao walipojaribu kulalamika.
Pamoja na hayo, Kamati hiyo imeipiga faini Simba SC kwa kitendo cha wapenzi na mashabiki wake kuwashambulia waamuzi baada ya mchezo huo kwa kuwarushia chupa za maji ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.
Katika kikao chake cha leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa mwishoni mwa wiki ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza, Kamati hiyo imemfungia beki Juma Nyoso wa Mbeya City kwa miaka miwili na kumpiga faini ya Sh Milioni 2, kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco.
Aidha, Yanga SC, imepigwa faini ya Sh 500,000 kufutia wachezaji wake watano, Salum Telela, Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa 'Barthez' na Donald Ngoma. kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa kanunu namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake watapata kadi zaidi ya tabo katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano.
Yanga SC pia imepigwa faini nyingine ya Sh 500,000 kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC mara baada ya mchezo kumalizika.
Taarifa ya TFF jioni hii, imesema kwamba mchezo namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union na Mwadui uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya mashabiki wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli la upande wa kaskazini walitoa  lugha ya matusi kwa waamuzi na kutishia kuwapiga na pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii Mohamed na jiwe moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika 3.
Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti wa wachezaji Coastal Union itatozwa faini ya Tsh 500,000/=
Mchezo namba 22 wa VPL kati ya Mtibwa Sugar na Ndanda uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu, Turiani. Ndanda hawakuleta watu wa kutosha kwenye pre match meeting hivyo wanapigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000/=)
Mchezo namba 23 wa VPL kati ya Simba SC na Kagera Sugar uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Simba walikuwa na wajumbe watatu na Kagera Sugar walikuwa na mtu mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote zimepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000).
Mchezo namba 17 wa VPL kati ya Stand united na African Sports kocha wa Stand United alitolewa nje ya eneo la ufundi kwa kutoheshimu taratibu za eneo hilo na pia alikataa kuongea na vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu wa kanuni namba 40 (11) anafungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mechi mbili na faini ya sh 500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.
Friends Rangers na KMC Mechi Na 8 Kundi A iliyofanyika uwanja wa Karume 27.9.2015. Timu ya KMC ya kinondoni ilifanya mabadiliko kwa kuingiza wachezaji 4 ambao ni kinyume cha kanuni. 
Kwa mujibu wa taarifa ya mwamuzi wachezaji waliofanyiwa mabadiliko ni Frank Mashoto badala ya Kudra Omar, Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon, Mfanyeje Mussa badala ya Kabange Mgunda na Sultani Kasiras badala ya Adam Said.
Kwa mujibu wa kanuni namba 14 (25) KMC imepoteza mechi na kupigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati anapewa onyo.

Nyosso afungiwa kucheza soka miaka miwili

Juma Said Nyosso, beki na nahodha wa kikosi cha Mbeya City anaetuhumiwa kumfanyia kitendo cha udhalilishaji mchezaji wa Azam FC John Bocco
Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.
Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.
Klabu ya Young Africans imepigwa faini ya shiligi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake watapata kadi zaidi ya tano katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano.
Wachezaji waliopata kadi za njano wa Young Africans katika mchezo huo ni Salum Telela, Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa na Mbuyu Twite.
Aidha klabu ya Yanga imepigwa faini nyingine ya shilingi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC mara baada ya mchezo kumalizika.
Mchezo utatazamwa tena ili kuangalia malalamiko ya Simba SC dhidi ya mwamuzi.
Simba pia inapigwa faini baada ya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwashambulia waamuzi baada ya mchezo ambapo waliwarushia chupa za maji ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.
Mchezo namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union na Mwadui uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya mashabiki wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli la upande wa kaskazini walitoa  lugha ya matusi kwa waamuzi na kutishia kuwapiga na pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii Mohamed na jiwe moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika 3.
Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti wa wachezaji Coastal Union itatozwa faini ya Tsh 500,000/=
Mchezo namba 22 wa VPL kati ya Mtibwa Sugar na Ndanda uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu, Turiani. Ndanda hawakuleta watu wa kutosha kwenye pre match meeting hivyo wanapigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000/=)
Mchezo namba 23 wa VPL kati ya Simba SC na Kagera Sugar uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Simba walikuwa na wajumbe watatu na Kagera Sugar walikuwa na mtu mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote zimepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000).
Mchezo namba 17 wa VPL kati ya Stand united na African Sports kocha wa Stand United alitolewa nje ya eneo la ufundi kwa kutoheshimu taratibu za eneo hilo na pia alikataa kuongea na vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu wa kanuni namba 40 (11) anafungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mechi mbili na faini ya sh 500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.
Friends Rangers na KMC Mechi Na 8 Kundi A iliyofanyika uwanja wa Karume 27.9.2015. Timu ya KMC ya Kinondoni ilifanya mabadiliko kwa kuingiza wachezaji 4 ambao ni kinyume cha kanuni. Kwa mujibu wa taarifa ya mwamuzi wachezaji waliofanyiwa mabadiliko ni
i. Frank Mashoto badala ya Kudra Omari
ii. Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon
iii. Mfanyeje Musa badala ya Kabange Mgunda na
iv. Sultani Kasiras badala ya Adam Said
Kwa mujibu wa kanuni namba 14 (25) KMC imepoteza mechi na kupigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati anapewa onyo.

Matokeo mechi zote za Ligi ya mabingwa Ulaya

UCL logo 
Usiku wa Septemba 30.9.2015 ilipigwa michezo nane ya UEFA Champions League (kombe la vilabu bingwa barani Ulaya) ilichezwa, mechi hizo zilishirikisha makundi manne tofauti kuanzia kundi E, F, G na H ambapo jumla ya timu 16 zilikuwa zikiumana kusaka pointi tatu ili kujiweka sawa kwa ajili ya kusonga mbele kwenye hatua inayofuta.
Matokeo ya michezo yote iliyopigwa usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano yapo kama ifuatavyo;
UCL Results 30.9.2015

Saturday, September 26, 2015

Unajua Luke Shaw kambiwa nini jamaa aliyemvunja mguu?

Luke Shaw 3 
Hector Moreno ameweka wazi kile ambacho ameambiwa na Luke Show alipokwenda Hospitali ambapo Shaw natibiwa siku ya Ijumaa iliyopita akiwa ameongozana na kocha wake Phillip Cocu.
Beki huyo wa kati wa PSV Eindhoven hakupewa adhabu yoyote licha ya kumuumiza Shaw kwa kumvunja mguu ambao atauuguza kwa miezi sita kabla ya kurejea uwanjani.
Moreno amesema: “kile kilichotokea kwa Shaw ilikuwa ni bahati mbaya. Na nilishtushwa sana”.
Luke Shaw 4 
“Nimefurahi nimeweza kuzungumza nae, niliongoza na Philip Cocu kwenda hospilali kumtembelea. Kitu ambacho kilikuwa ni kigumu kwa mwanzoni, lakini alinipokea vizuri na hakunilaumu”.
“Aliangalia picha na akasema ilikuwa ni sehemu ya mchezo. Kiauli hiyo ilinifanya nitabasamu”.
Shaw alirejea Manchester siku ya Jumapili asubuhi akitokea Uholanzi ambako alikuwa anatibiwa mguu wake wa kulia uliovunjika mara mbili wakati timu yake ikipambana na PSV kwenye mchuano wa kombe la klabu bingwa Ulaya.
Luke Shaw 6 
Kwenye posti yake ya Jumamosi kwenye account ya Istagram mlinzi huyo wa aliwashukuru wafanyakazi wa hospitali ya St Anna Hospital mjini Eindhoven.
Aliposti picha tatu akiwa pamoja na wafanyakazi hao zilizoambatna na ujumbe uliosomeka: ‘I just wanna say a massive thank you to everyone at St Anna hosptal for all the care and attention they have given me the last few days’. (Namshukuru kila mmoja kwenye hospitali ya St Anna kwa uangalizi walionipa siku chache zilizopita).
Luke Shaw 5

Mahaka ya Brazil imezuia mali za Neymar

sdsfds
Mahakama ya Brazil imezuia mali za mchezaji wa Barcelona Neymar ambazo zina thamani ya $48 million. Mahakama ya huko Sao Paulo imetangaza ijumaa hii mali za mchezaji huyu mwenye miaka 23 ana makosa ya kukwepa kodi ya kiasi cha $16m kati ya mwaka 2011 na 2013.
Neymar alihamia Barcelona akitokea Santos kwa kiasi cha pesa ambacho bado kinafanyiwa uchunguzi na asasi za Hispania kuhusu swala la kodi kwasababu wanadhani kuna udanganyifu ulifanyika.
Jaji Carlos Muta ametangaza kwamba mali zenye thamani ya $5m zitashikiliwa hadi pale swala la kodi litakapowekwa sawa. Neymar amepewa agizo la kulipa kodi na faida juu kutokana na kosa hilo.

Pele ataja timu ambayo angecheza England

Pele

Nguli wa soka ulimwenguni, Pele amesema kama angepata fursa ya kucheza ligi kuu nchini Uingereza, basi angekipiga kunako klabu ya Arsenal.
Pele amedai kuwa mtindo wanaocheza Barcelona unafafana sana timu yake ya zamani ya Santos, ambayo aliichezea kati ya mwaka 1956 na 1974.
Alipoulizwa ni timu gani angependa kucheza nchini Uingereza, Pele alijibu.
“Arsenal ingekuwa ndio sehemu pekee ambayo ningeweza kucheza”,  Pele aliliambia gazeti la Telegraph .
“Napenda sana timu ambazo hucheza mchezo wa kujiachia/kufunguka uwanjani. Kwa sasa ni vigumu mno kusema ni timu gani ambayo inacheza mchezo huo.
Bosi: Pele angejikuta kwa sasa akiwa chini ya Arsene Wenger
Pele anasema staili ya Barcelona inakaribiana na ile ya timu yake ya zamani ya Santos”.
“Kati ya Chelsea na Arsenal? Ningependa kucheza Arsenal kama ningepata hiyo fursa”.

Wajue wakali wa mabao matano kama Lewandowski


Robert 

Nikiwa naamini hali yako ni njema, mimi pia ni mzima kiasi ila nasikitika yanayotokea pale Saudia huku nikiwaombea Marehemu wote wawe salama huko waliko. Tukirejea katika soka, naamini habari ya mujini ni Lewandowski hasa baada ya kufunga magoli 5 pale timu yake ya Bayern Munich ilipo toa kisago cha 5-1 dhidi ya timu ngumu ya Wolfsburg. Kutokana na hili leo nimekuwekea listi ya Wachezaji wengine ambao wamewahi kufunga magoli 5 katika mechi 1, karibu sana kuungana na mimi hapa chini…
ROBERT LEWANDOWSK
Huyu jamaa ni mchezaji hatari sana ambaye kufunga goli inawezekana ndiyo kazi rahisi kuliko hata kuvuta pumzi. Aliwahi kuwafunga Real Madrid magoli 4 kwenye UEFA na hapo dunia ya soka ikaamini kuwa huyu jamaa anaweza kutoa dozi kubwa zaidi endapo atapewa upenyo wa kufanya hivvo. Baada ya Wolfsburg kujichanganya kwenye mechi ya Bundesliga siku kadhaa zilizopita, Lewandowski alitupia magoli 5 peke yake tena ndani ya dakika 9 huku akikamilisha ‘hat trick’ yake ndani ya dakika 3 na sekunde 22. Kumbuka aliyafanya haya baada ya kutokea benchi huku Bayern ikiwa nyuma kwa goli moja.
LUIZ ADRIANO
luiz-adriano 
Ni kijana mdogo ambaye hivi karibuni aliandika rekodi ya kufunga magoli 5 katika mechi 1 ya UEFA. FC BATE Borisov ilimruhusu Adriano kufunga magoli 5 mwaka 2014 wakati Shakhtar Donetsk ilipocheza na timu hii na kushinda magoli 7 huku Mbarizil huyu akitupia magoli 5 kwenye usiku wa UEFA na kuandikwa kwenye vitabu vya historia sambamba na mchezaji bora wa Ulaya Lionel Messi ambaye tayari alishawahi kufanya hivi kipindi cha nyuma. Luiz Adriano licha ya kufunga magoli haya, hakufanikiwa kuwa mfungaji bora wa Ulaya kwa kipindi cha 2014.
MIROSLAV KLOSE
Miroslav-Klose 
Ni Mchezaji mwenye busara sana ila Bologna hawatamsahau mwaka 2013 pale ambapo Klose alifunga magoli 5 katika ushindi wa 6-0 walioupata Lazio kwenye mechi ya ligi kuu ya Italia. Klose ni mmaliziaji mzuri sana japokuwa hakujaaliwa chenga wala mbio ila amepewa macho ya ziada ya kutambua nyavu zilipo. Hadi sasa Klose anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kumpiku nguli wa soka Ronaldo de Lima.
FERNANDO MORIENTES
Morientes 
Naamini Liverpool wanamfahamu vyema kwani ameshacheza Anflied na kushindwa kuwika kama alivyokuwa Hispania. Las Palmas walifungwa 7-0 na Real Madrid mwaka 2002 huku Morientes akitia kambani magoli 5 na kuwa miongoni mwa Wanasoka waliocheza Madrid na kutupia magoli 5 katika mechi 1. Katika mechi hii nakumbuka Morientes alikosa nafasi ya kutupia magoli 6 baada ya kukosa mkwaju wa penati.
ALAN SHEARER
alan shearer
Hakuna asiyefahamu makubwa aliyofanya huyu jamaa katika ligi kuu ya Uingereza. Mwaka 1999, Newcastle iliinyuka Sheffield Wednesday 8-0 huku Shearer akiingia nyavuni mara 5. Japokuwa alifunga penati 2 katika magoli yake ila hadi sasa Shearer anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote katika ligi kuu ya Uingereza na timu yake ya Newcastle.
OLEG SALENKO
5 Jul 1994: HRISTO STOITCHKOV OF BULGARIA CELEBRATES THE FIRST GOAL DURING THE FIRST HALF OF THE SECOND ROUND 1994 WORLD CUP MATCH AGAINST MEXICO AT GIANTS STADIUM IN EAST RUTHERFORD, NEW JERSEY.
Japokuwa wengine tulikuwa kwenye ‘Mabeseni’ ila Ulimwengu wa digitali unatuwezesha kumfahamu huyu jamaa zaidi. Salenko aliwafunga Waafrika magoli 5 baada ya Urusi kuibamiza Cameroon magoli 6-1 kwenye michuano ya kombe la dunia pale Marekani. Hadi sasa rekodi hii haijavunjwa katika michuano hii licha ya miaka 20 kupita tangu Mshambuliaji huyu kufanya unyama huu kwa Waafrika na kuidhihirishia Dunia kuwa Afrika kisoka bado sana. Kutokana na magoli yake, Salenko alifanikiwa kuwa mfungaji bora wa michuano hii ambayo Brazil ilifanya makubwa.
JERMAIN DEFOE
Defoe 
Akiwa katika ubora wake mwaka 2009, Defoe alitupia magoli 5 pale timu yake ya Spurs iliposhinda 9-1 dhidi ya Dearby Country. Defoe alicheza kwa mafanikio ya wastani katika timu ya Spurs kitu ambacho kilimsaidia kuweka rekodi hii ya kiume ambayo kila mchezaji anatamani kuitekeleza kabla hajastaafu.
LIONEL MESSI
lionel-messi-barcelona-la-liga3248555-1425893997-2343424 
Alifanya makubwa kwenye usiku wa Uefa mwaka 2012 pale ambapo wachezaji wa Bayer Leverkusen walipompa uhuru na kusahau makali ya mchezaji huyu ambaye inasadikika ndiye bora kuwahi kutokea hapa Duniani. Barcelona iliiadhibu Leverkusen magoli 7-1 kwenye mzunguko wa pili wa hatua ya 16 bora huku Mchawi Messi akimpa kazi mlinda mlango wa Leverkusen kuokota mipira mara 5. Kutokana na magoli haya, Messi alikuwa Mchezaji wa kwanza kufunga magoli 5 katika mechi moja ya UEFA.
RADAMEL FALCAO
Falcao 2 
Anabezwa sana kwa sasa ila ni Mchezaji aliyeweka rekodi nyingi wakati akiwa katika ubora wake. Ikumbukwe Mwaka 2012 akiwa Atletco de Madrid, Falcao aliwafunga Deportivo la Coruna magoli 5 pale ambapo ‘Superdepo’ walilala 6-1 kwenye La liga. Falcao alikuwa mchezaji hatari ambaye anawaumiza akili mabeki wa timu pinzani kutokana na utaalamu wake wa kufumania nyavu. Kwa sasa yupo Chelsea na bado anadharaulika kutokana na kushuka kiwango.
DIMITAR BERBATOV
Dimitar Berbatov 
Baada ya kuondoka Spurs na kwenda United, hatimaye Mchezaji huyu akiwa Old Trafford alitupia magoli 5 pale ambapo United iliinyuka Blackburn Rovers magoli 7-1. Mbulgaria huyu hakupata mafanikio sana akiwa na uzi mwekundu wa United licha ya kufahamika kama miongoni mwa wamaliziaji wazuri hadi sasa licha ya umri wake kusogea.
CRISTIANO RONALDO
ronaldo 
Huyu jamaa mimi namuheshimu na kumuogopa sana kwani anaamua afunge magoli mangapi katika mechi gani. Cr7 ana uwezo wa kufunga idadi yoyote ya magoli atakayo. Miezi michache iliyopita Madrid ilishinda 9-1 dhidi ya Granada huku Cr7 akiingia nyavuni mara 5 na kuendelea kuandika rekodi mbalimbali ikiwemo ile ya kufunga ‘hat-trick’ ndani ya dakika 18. Ronaldo ni mchezaji hatari ambaye kwa sasa anainyemelea rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote pale Real
Madrid.

Wednesday, September 23, 2015

Ubabe wa Coast dhidi ya Arsenal wamtokea puani, FA kumfungia

Diego Costa vs Gabriel 1
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa anaweza kupewa adhabu ya hadi mechi tatu na chama cha soka nchini England baada ya mchezo usio wa kiuungwana kwa mlinzi wa Arsenal Laurent Koscienly katika mchezo wa jumamosi iliyopita.
Katika mchezo huo uliomalizika kwa Chelsea kushinda mabao 2-0 dhidi ya Arsenal, ulimalizika kwa Arsenal kuwa na wachezaji wawili pungufu waliooneshwa kadi nyekundu na mwamuzi Mike Dean.
Costa ambaye anakabiliwa na adhabu kwa mchezo mbaya kwa Koscienly alioneshwa kadi ya njano na mwamuzi Mike Dean ambaye hata hivyo haikujulikana kadi hiyo ni kwa kosa la Koscienly au ni majibizano yake na Gabriel Paulista ambaye pia alioneshwa kadi nyekundu baada ya kuingia katika mtego wa Costa.
Diego Costa va Gabriel 
FA waliipitia ripoti yenye utata ya mwamuzi Mike Dean ambaye hakumuadhibu Diego Costa kwa kitendo hicho kwa madai ya kutoona uzuri kilichotokea.
FA pia wamempa adhabu Gabriel Paulista kwa kitendo chake kilichopelekea kupigwa kadi nyekundu, wakati Saint Carzola akipewa onyo kali, na klabu zote mbili za Arsenal na Chelsea zikipigwa faini kwa kutowafunza adabu wachezaji wake. Wote wamepewa hadi saa kumi na mbili jioni jumanne hii kukata rufaa.
Diego Costa 1

Ferguson awataja wachezaji wanne bora kuwahi kuwafundisha

Man utd 4 
Kocha mstaafu wa Manchester United Sir Alex Ferguson katika kitabu chake kipya cha hivi sasa, amewataja wachezaji wanne wa kiwango cha dunia kuwahi kuwafundisha.
Alex Ferguson amemtaja Cristiano Ronaldo kuwa ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kumfundisha huku akiwaongeza Erick Cantona, Ryan Giggs na Paul Scholes kama wachezaji wake bora wa kiwango cha dunia.
Man utd 42 
Alex anasema, “katika kitabu changu kuna wachezaji wawili tu wa kiwango cha dunia ambao bado wanacheza hadi sasa, Ronaldo na Messi”.
Man utd 41 
Katika orodha hiyo hakuna majina ya wachezaji Wayne Rooney, David Beckham wala Rio Ferdinand.
Lakini Fergie anasema aliowataja, wamethibitisha ubora wao huku akimwagia sifa Ryan Giggs kwamba atakuja kuwa ni kocha mkubwa na mafanikio mengi siku moja.
Akiongea kuhusu kitu anachokijutia katika maisha yake ya ukocha, Fergie anasema ni kutokushinda mataji mengi ya Ulaya ingawa alishinda makombe mbalimbali ya nyumbani.
Man utd 43

Gabriel ashinda kesi, lakini bado majanga

Gabriel 
Mlinzi wa Arsenal Gabriel ameshinda rufaa yake baada ya klabu yake kupeleka ushahidi wa picha za video kumtetea mlinzi huyo.
Mwamuzi Mike Dean aliyechezesha mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal Jumapili iliyopita, alimtoa nje kwa kadi nyekundu beki huyo raia wa Brazil akidaiwa kumganyaga kwa nyuma mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa lakini picha za video zilizopelekwa kama ushahidi kwenye chama cha soka cha England (FA) hazioneshi kama Costa aliguswa na mguu wa Gabriel.
Chama cha soka nchini England kiliendelea kusubiri hadi saa 12 jioni siku ya Jumanne kuona kama Costa atawasilisha rufaa yake lakini haikuwa hivyo na kupitisha adhabu ya kumfungia mechi tatu.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho tayari ameshaamua kumtumia Radamel Falcao kwenye mechi dhidi ya Walsall siku ya Jumatano kwenye mchezo wa kombe la Capital One.
Lakini wakati huohuo, Gabriel bado anakabiliwa na kesi ya utovu wa nidhamu aliounesha mara baada ya kuoneshwa kadi nyekundu na Mike Dean huku akionekana kutaka kugoma kutoka nje ya uwanja.
Lakini maamuzi hayo yanamaanisha Gabriel atacheza mchezo wa Capita One siku ya Jumatano dhidi ya Tottenham.

Lewandoski apiga bao 5 akitokea benchi na kuweka rekodi

Robert 
Wakati Bayern Munich ikiwa nyuma kwa goli 1-0 hadi mapumziko kwenye uwanja wake wa nyumbani, Robert Lewandowski aliingia akitokea benchi na kubadilisha matokeo ya mchezo huo kwa kufunga magoli matano ndani ya dakika tisa kwenye mchezo dhidi ya Wolfsburg uliomalizika kwa Bayern kuibuka na ushindi wa goli 5-1.
Mabingwa hao wa Bundesliga waliingia kwenye mechi hiyo dhidi ya Wolfsburg ambayo ilimaliza ikiwa nafasi ya pili msimu uliopita walianza kuduwazwa kwa goli la Daniel Caligiuri la kipindi cha kwanza na kumfanya Pep Guardiola kufanya mabadiliko mwanzoni mwa kipindi cha pili.
Kocha huyo wa Bayern alimpumzisha kiungo Thiago AlcƔntara na kumuingiza Lewandowski.
Mkali huyo mwenye miaka 27 ilimchukua dakika sita pekee kuisawazishia Bayern baada ya kuunasa mpira kutoka kwa mchezaji mwenzake wa zamani Dante na kuiandikia Bayern bao la kusawazisha kabla ya kuiweka timu yake mbele dakika moja baadae kwa shuti kali la nje ya boksi.
Lewandowski alikamilisha hat-trick yake dakika nne baadae na kuweka rekodi ya kuwa hat-trick ya haraka zaidi kufungwa kwenye historia ya Bundesliga. Rekodi ya hat-trick ya mapema ilikuwa ikishikiliwa na Michael Toennies iliyowekwa mwaka 1991 ndani ya dakika sita. 
Rekodi yake ya mabao matano kwenye mechi moja ni ya haraka zaidi mara nne ya ile iliyowekwa na Jermain Defoe mwaka 2009 Tottenham iliposhinda kwa goli 9-1 dhidi ya Wigan.
Dakika mbili baadae baada ya kufunga hat-trick, Lewandowski alifunga goli la nne akiunganisha krosi ya mchezaji mpya aliyesajiliwa kwenye klabu hiyo Douglas Costa kabla hajapiga goli la tano kwa staili ya ‘bicycle kick’ akiwa nje kidogo ya boksi na kumwacha Guardiola akitabasamu.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Borussia Dortmund anakuwa mchezaji wa kwanza wa Bayern kufunga magoli matano ndani ya Bundesliga tangu alipofanya hivyo Dieter Hoeness mwaka 1984.
Lewandowski pia amekuwa mchezaji wa kwanza aliyetokea benchi na kufunga magoli matano.

Ligi daraja la kwanza yadhaminiwa an Star Times

Mkurugenzi mkuu wa Star Times Llao Lan Fang (kuhoto) na Rais wa TFF Jamal Malinzi wakisaini mkataba wa udhamini wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara
Mkurugenzi mkuu wa Star Times Liao Lan Fang (kuhoto) na Rais wa TFF Jamal Malinzi wakisaini mkataba wa udhamini wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limesaini mkataba wa udhamini wa ligi daraja la kwanza (FDL) na kampuni ya Star Times Media wenye thamani ya shilingi milioni miatisa za kitanzania kwa muda wa miaka mitatu ili kusaidia gharama za uendeshaji wa ligi hiyo.
Utiaji saini huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Kisenga Millennium Towers, Makumbusho kati ya TFF na Star Times.
Llao Lang Fang akibadilishana mkataba na  Rais wa TFF Jamal Malinzi
Liao Lang Fang akibadilishana mkataba na Rais wa TFF Jamal Malinzi
Rais wa TFF Jamal Malinz ameishukuru Star Times kwa kukubali kudhamini ligi hiyo ili kuzisaidia timu shiriki  kujikimu pamoja na bodi ya ligi kuwalipa waamuzi pamoja na garama nyingine za uendeshaji wa ligi hiyo ambazo zimekuwa zikibebwa na TFF kwa miaka yote.
Malinzi amesema, kila timu itapata shilingi milioni 15. Milioni 10 kati ya hizo inatoka moja kwa moja Star Times wakati milioni tano itatoka kwenye haki za matangazo ya television kutokana na ligi hiyo kuonekana moja kwa moja (live) kupitia ving’amuzi vya Star Times.
Rais wa TFF Jamal Malinzi (kulia) pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Star Times Media Llao Lan Fang wakionesha mkataba wa udhamini wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara
Rais wa TFF Jamal Malinzi (kulia) pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Star Times Media Liao Lan Fang wakionesha mkataba wa udhamini wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara
Hata hivyo Malinzi amefafanua kuwa, mkata uliosainiwa leo ni wa udhamini wa ligi kutoka Star Times lakini wiki ijayo watasaini mkataba mwingine na kampuni nyingine itakayopewa haki ya kurusha matangazo ya mechi za ligi daraja la kwanza.
KUTOKA KUSHOTO: Mkurugenzi wa masoko Star Times Zuhura Hanif, Mkurugenzi mkuu Star Times Liao Lan Fang, Rais wa TFF Jamal Malinzi na Meneja masoko wa TFF Peter Simon
KUTOKA KUSHOTO: Mkurugenzi wa masoko Star Times Zuhura Hanif, Mkurugenzi mkuu Star Times Liao Lan Fang, Rais wa TFF Jamal Malinzi na Meneja masoko wa TFF Peter Simon
Liao Lan Fang ambaye ni mkurugenzi mkuu wa Star Times amesema, mbali na udhamini huo wa shilingi milioni miatisa, vilabu hivyo vitapta fursa ya kuonekana moja kwa moja kwenye nchi zaidi ya 10 za Afrika ambapo Star Times inapatikana.
Waandishi wa habari wakifanya kazi yao
Waandishi wa habari wakifanya kazi yao

Malinzi aota kombe la Dunia

Jamal Malinzi, Rais wa TFF
Jamal Malinzi, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Jamal Malinzi ameendelea kusisitiza kwamba Tanzania itashiriki michuano ya kombe la dunia miaka ijayo kutokana na maandalizi ambayo tayari yameanza kufanywa na shirikisho hilo kwa kuanza kujenga timu za vijana.
Pia katika hilo Malinzi ameongeza kwamba, tayari wameshaomba na kukubaliwa kuandaa michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana wa U17 michuano inayotarajiwa kufanyika mwaka 2019 huku akisisitiza tayari timu kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo imeshaanza kuanaliwa.
Malinzi ametoa kauli hiyo leo wakati akifunga kozi ya makocha wa leseni C ya CAF iliyokuwa ikifundishwa na Salum Madadi ambaye ni mkurugenzi wa ufundi wa TFF.
“Sisi kama TFF tumesema kwamba mwaka 2020 tutacheza fainali za Olympic za Tokyo tumesema hivyo na tunaomba Mungu atusaidie”, amesema Malinzi.
“Kama tukiweza kufanikiwa 2020, tukacheza fainali za Olympic Tokyo, 2026 tutakuwa na timu ya na timu ya kucheza kombe la dunia mwaka 2026”.

Yanga wasalimu amri, kusaini mkataba na Azam TV


HATIMAYE Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji amemaliza tofauti zake na kampuni ya Azam TV na kukubali klabu kusaini mikataba yote ya kampuni hiyo, mali ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake.
Habari ambazo mwanasokablog.com imezipata kutoka ndani ya Yanga SC, ni kwamba klabu hiyo sasa inatarajiwa kusaini Mkataba wa haki za Televisheni wa Azam FC na pia wa kipindi cha Yanga TV, ambayo kwa pamoja itawafanya wapokee si chini ya Sh. Milioni 600 za ‘chap chap’.
Mechi za Yanga SC zimekuwa zikionyeshwa kama kawaida na Azam TV, lakini kwa miaka yote miwili klabu haijachukua mgawo wake Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Julai 29, mwaka 2013 Manji alipinga vikali TFF na Bodi ya Ligi kuamua peke yao kuingia Mkataba wa miaka mitatu Azam TV akidai haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani.
Lakini pamoja na madai hayo, kuna mpango hasi wa ushirikiano baina ya na Simba na Yanga kwenda kusaini Mkataba na kampuni moja ya Kenya iliyopanga kuitibulia Azam TV.
Lakini kutokana na TFF chini ya Rais Leodegar Chillah Tenga wakati huo kusimama kidete kuitetea Azam TV iliyoweka historia katika soka ya Tanzania kwa dau lake nono, mpango huo ukafa.
Simba SC walikubali yaishe na kusaini hadi Mkataba wa kipindi cha TV ambao uliwafanya wapatiwe Sh. Milioni 331 za Mkataba wa miaka mitatu.
Yanga SC itakaposaini mikataba ya Azam TV pamoja na kupewa mgawo wa matangazo ya Ligi Kuu takriban Sh. Milioni 300 za miaka miwili, watalipwa pia na fedha za Yanga TV kwa sababu hayo ni makubaliano ya kimsingi kabla ya kusainiwa Mkataba huo.

Saturday, September 19, 2015

Morata akataa kuondoka Juve kwenda Real Madrid




MSHAMBULIAJI wa Juventus, Alvaro Morata amekanusha uvumi ulioneea kwamba anaweza kurudi Real Madrid wakati wa majira ya joto yajayo baada ya kubainisha kuwa kwa sasa amejikita katika klabu yake ya sasa.
Morata aliondoka Madrid na kujiunga Juventus msimu uliopita, lakini Klabu hiyo ya Hispania  imesema inaweza kumsajili mchezaji huyo kwa ada inayotajwa kuwa ni euro milioni 25 mwishoni mwa msimu wa 2015-16.
Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Hispania, ambaye amefunga magoli 15 katika mashindano yote kwa Juve msimu uliopita na kuuiwezesha kushinda taji lake la nne mfululizo la Ligi Kuu ya Italia, Scudetto na kufika fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya, amesisitiza anafuraha kubakia Turin.
“Hakuna jinsi, Juventus ni timu yangu niko safi hapa,” alisema Morata wakati alipoulizwa na gazeti la Sport Mediaset kama anashauku ya kurudi Real.
“Sifikirii kuhusu kuondoka katika Klabu hii.”
Morata aliongeza katika mahojiano na Sky Sports Italia: “Nakubali kwamba, Madrid wanahitaji mimi, lakini kwa sasa akili yangu ni kufunga na kushinda kila kitu kinachowezekana nikiwa na Juventus.”
Juve ambayo imeaanza Ligi Kuu ya Italia, Serie A, bila ushindi katika mechi tatu lao Jumapili itacheza na Genoa.

Amokachi aacha kazi baada ya wiki tano




NAHODHA wa zamani wa Nigeria, Daniel Amokachi amejiuzulu wadhifa wake kama meneja wa klabu ya ligi kuu ya Nigeria, FC IfeanyiUbah baada ya kuiongoza kwa wiki tano pekee.
Amokachi mwenye umri wa miaka 42 alikuwa awali ameeleza hamu yake ya kutaka kushinda mataji na kuhakikisha klabu hiyo.
Lakini ameamua kuondoka baada ya msururu wa matokeo mabaya na kutoelewana kati yake na mmiliki wa klabu hiyo.
“Nasikitika kuondoka baada ya kipindi kifupi hivi, lakini kandanda inaendelea,” alisema Amokachi akiiambia BBC Sport.
“Nilikuwa shabiki wa Klabu hii kabla ya kuteuliwa kwangu kama meneja kwa sababu ya msingi uliopelekea kuundwa kwake.
"Lakini sasa naitakia kila la heri na nitafuatilia hatua wanazopiga kwa fahari kuu.”
Ripoti zimedokeza kuwa Amokachi hakufurahishwa na sera ya klabu hiyo ya kutumia barabara hatari usiku kurejea nyumbani baada ya kucheza mechi za ugenini.
Msimamo wake ulimfanya kukosana na milionea anayemiliki klabu hiyo, Ifeanyi Ubah.
Mfanyabiashara huyo anaaminika kuchukulia hatua ya kocha huyo kuwa kukaidi mamlaka yake.
Amokachi alikataa kusema lolote alipoulizwa kuhusu suala hilo.
“Soka haitabiriki na hakuna wakati wa kwenda mbele na nyuma,” alisema.
"Imekuwa heshima kubwa kuhusika katika kilabu hii lakini kwa sasa safari yangu imefikia kikomo FC IfeanyiUbah."

Liverppol yaanza kwa sare Ligi ya Europa


MATOKEO MECHI ZA JANA UEFA EUROPA LEAGUE 
Asteras Tripolis 1 - 1 Sparta Prague 
APOEL Nicosia 0 - 3 FC Schalke 04 
Dnipro Dnipropetrovsk 1 - 1 Lazio 
Sporting Lisbon 1 - 3 Lokomotiv Moscow 
Skenderbeu Korce 0 - 1 Besiktas
Fiorentina  1 - 2 FC Basel
Tottenham Hotspur 3 - 1 FK Qarabag
Athletic Club 3 - 1 FC Augsburg
Lech Poznan 0 - 0 Belenenses
Partizan Belgrade 3 - 2 AZ
Ajax 2 - 2 Celtic
Viktoria Plzen 2 - 0 Dinamo Minsk
Napoli 5 - 0 Club Brugge
Bordeaux  1 - 1 Liverpool
FK Qabala 0 - 0 PAOK Salonika
FC Sion 2 - 1 Rubin Kazan
Slovan Liberec  0 - 1 Sporting Braga
SK Rapid Wien 2 - 1 Villarreal
Borussia Dortmund 2 - 1 FK Krasnodar
FC Groningen 0 - 3 Marseille
Fenerbahce 1 - 3 Molde
FC Midtjylland 1 - 0  Legia Warsaw
Kiungo wa Liverpool, Adam Lallana (kushoto) akipambana na Nicolas Maurice-Belay wa Bordeaux (kulia) katika mchezo wa Europa League jana

LIVERPOOL wamelazimisha sare ya 1-1 na Bordeaux ugenini katika mchezo wa Kundi B UEFA Europa League usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Matmut Atlantique, Ufaransa.
Adam Lallana alianza kuifungia Liverpool mjini Bordeaux dakika ya 65, kabla ya Jussie Ferreira Vieira kusawazishia wenyeji dakika ya 81.
Timu nyingine ya England, Tottenham Hotspur imeanza vyema kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya FK Qarabag mchezo wa Kundi J Uwanja wa White Hart Lane, London, mabao yake yakifungwa na Heung-Min Son dakika ya 28 na 30 na Erik Lamela dakika ya 86, huku wageni wakipata bao lao kwa penalti dakika ya saba kupitia kwa Richard Almeida.Fenerbahce striker Robin Van Persie was unable to add to his single goal since joining from United
Mshambuliaji wa Fenerbahce, Robin Van Persie alishindwa kufunga jana 

Mchezo mwingine wa kundi hilo, RSC Anderlecht imetoa sare ya 1-1 na Monaco bao likifungwa Guillaume Gillet dakika ya 11, kabla ya Lacina Traore kusawazisha dakika ya 85 Uwanja wa Constant Vanden Stockstadion.
Kundi K, FC Schalke ya Ujerumani imeshinda 3-0 ugenini dhidi ya APOEL Nicosia Uwanja wa GSP nchini Cyprus mabao ya Joel Matip dakika ya 28 na Klaas-Jan Huntelaar dakika ya 35 na 71.
Lazio imelazimisha sare ya 1-1 ugenini na Dnipro Dnipropetrovsk  katika mchezo wa Kundi G, bao lao likifungwa na Sergej Milinkovic-Savic dakika ya 34 kabla ya wenyeji kusawazisha dakika ya 90 na ushei kupitia kwa Evgen Seleznyov Uwanja wa Dnipro Arena.
Monaco 
Fiorentina imechapwa 2-1 katika mchezo wa Kundi I na FC Basel licha ya kuongoza kwa 1-0 hadi mapumziko kwa bao la Nikola Kalinic dakika ya tatu, kwani kipindi cha pili Birkir Bjarnason aliwasawazishia ugenini ya 71 na Mohamed Elneny akafunga la ushindi dakika ya 79 Uwanja wa Artemio Franchi.
Tottenham head coach Mauricio Pochettino opted to ring the changes for his side's Europa League opener with QarabagĀ 
Kikosi cha Tottenham kilichoiadhibu Qarabag jana