Baada ya picha nyingi na taarifa
kuzagaa zinazomhusu mchezaji wa zamani wa vilabu vya Yanga, Simba pamoja
na Coastal Union Nsa Job akiwa amelazwa hospitali kufuatia kujeruhiwa
vibaya na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CHADEMA, imetoka taarifa
kuwa hali yake inaendelea kuwa nzuri.
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa
wa Kilimanjaro Goodluck Moshi amesema hali ya Nsa Job anaendelea vizuri
akiwa bado amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi lakini tayari
ameondolewa mashine za kumsaidia kupumua.
“Taarifa iliyopo ni kwamba,
alipigwa (Nsa Job) na jiwe kubwa kichwani wakati akiwa kwenye gari
akitokea nyumbani kwa mgombea ubunge Manispaa ya Moshi kupitia Chama Cha
Mapinduzi Ndugu Davis Mosha”, Moshi ametaarifu .
“Wakati wanatoka nyumbani kwa
Mosha wakiwa kwenye gari yeye (Nsa Job), Mosha na mtu mwingine,
walipofika barabarani, likarushwa jiwe kubwa likapita kwenye kioo cha
dirisha na kumpasua kwenye kichwa na taya, akakimbizwa KCMC amefanyiwa
upasuaji bado yupo ICU lakini hali yake inaendelea vizuri”.
“Ameshaondolewa mashine za
kupumulia na anaweza kuongea hivi sasa, ni jambo la kumshukuru Mungu
kutokana na hali halisi ilivyokuwa imejitokeza”.
Jana kuna picha zilienea kwenye
mitandao ya kijamii zikionesha kuwa Nsa Job amelazwa kwenye wodi ya
wagonjwa mahututi (ICU) baada ya kujeruhiwa vibaya kwenye eleo la
kichwa.
No comments:
Post a Comment