Mshambuliaji
wa klabu ya Manchester United Anthony Martial ametwaa tuzo ya mchezaji
bora wa mwezi Septemba ikiwa ni tuzo ya kwanza kwa mchezaji wa
Manchester United kwenye ligi kuu England chini ya kocha Louis van Gaal
tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2014.
Martial amecheza michezo minne
kwenye ligi kuu ya England na tayari ameshafunga magoli matatu,
Manchester United itacheza na Everton kwenye uwanja wa Goodson Park.
Kinda huyo wa Kifaransa alitua
Old Trafford akitokea Monaco kwa ada ya uhamisho wa pauni 36 huku kukiwa
na kipengele cha kuongezeka hadi pauni milioni 58.
Martia aliunga goli lake la
kwanza dhidi ya Liverpool alipotokea benchi ambapo United iliibuka na
ushindi wa goli 3-1. Mchezo kati ya Manchester United dhidi ya
Southampton, Martial alifunga mgoli mawili wakati Manchester iliposhinda
kwa goli 3-2.
Wakati Martial akichukua tuzo ya
mchezaji bora wa mwezi Septemba, kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino
amechukua tuzo ya kocha bora wa mwezi wa tisa.
No comments:
Post a Comment