MWANASOKA
bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amefanyiwa pati la kuweka rekodi ya
kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Real Madrid katika sherehe
zilizofanyika Uwanja wa Santiago Bernabeu na kuhudhuriwa na wachezji
wenzake.
Ronaldo
aliyevishutumu vyombo vya habari kwa kumsakama, alijumuika na wachezaji
wenzake kama Gareth Bale, Karim Benzema na Marcelo waliompogeza Mreno
huyo mwenye umri wa miaka 30 katika pati ambayo mama yake, pamoja na
mwanawe na wakala wake, Jorge Mendes walihudhuria pia.
Pamoja
na hayo taarifa rasmi zinasema Ronaldo amefikia rekodi ya mfungaji bora
wa kihistoria wa klabu hiyo, Raul aliyefunga mabao 323 sawa na Ronaldo
Ronaldo akiwa na mama yake, Dolores huku mwanawe Cristiano Ronaldo Jr akishuhudia wakati akipokea tuzo yake kiatu na mpira wa Fedha
No comments:
Post a Comment