Saturday, October 3, 2015

Nani na nani kwenda fainali michuano ya Afrika 2015

RATIBA LIGI YA MABINGWA AFRIKA
Oktoba 3, 2015
USM Alger (Algeria) Vs Al Hilal (Sudan)
Oktoba 4, 2015
TP Mazembe (DRC) Vs El Merreikh (Sudan)
MATOKEO MECHI ZA AWALI
Septemba 27, 2015  
Al Hilal (Sudan) 2-1 USM Alger (Algeria)
Septemba 26, 2015  
Al Merreikh (Sudan) 2-1 TP Mazembe (DRC)
RATIBA KOMBE LA SHIRIKISHO
Oktoba 3, 2015
Zamalek (Misri) Vs ES Sahel (Tunisia)
Oktoba 4, 2015
Al Ahly (Misri) Vs Orlando Pirates
MATOKEO MECHI ZA AWALI
Septemba 27, 2015  
ES Sahel (Tunisia)  5-1 Zamalek (Misri)
Septemba 26, 2015  
Orlando Pirates 1-0 Al Ahly (Misri)
Wanzania wa TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (katikati) kesho watawania kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa 

TIMU zitakazokutana kwenye fainali za michuano ya klabu barani Afrika zinatarajiwa kupatikana wikiendi hii.
Katika Ligi ya Mabingwa leo, USM Alger ya Algeria watakuwa wenyeji wa El Hilal ya Sudan, wakati kesho Tout Puissant Mazembe ya DRC wataikaribisha El Merreikh ya Sudan pia.
Katika Kombe la Shirikisho, leo Zamalek ya Misri itaikaribisha Etoile du Sahel ya Tunisia, wakati kesho Al Ahly ya Misri pia itakuwa mwenyeji wa Orlando Pirates.
Mechi za awali USM Alger ilishinda 2-1 dhidi ya El Hilal, wakati El Merreikh iliifunga 2-1 TP Mazembe-  na katika Kombe la Shirikisho, Etoile du Sahel iliitandika mabao 5-1 Zamalek na Pirates waliilaza 1-0 Al Ahly.
Etoile pekee ndiyo inapewa nafasi ya kutangulia Fainali kutokana na ushindi mnono katika mchezo wa kwanza mjini Sousse, Tunisia, lakini mechi nyinine zote hakuna anayeweza kuthubutu kutabiri.
Na labda kidogo USM Alger baada ya ushindi wa ugenini wa 2-1, kidogo nao wanapewa nafasi ya kumalizia vizuri nyumbani.
Lakini Merreikh na Pirates hakika watakuwa na shughuli pevu wote baada ya ushindi mwembamba nyumbani. Mazembe wanahitaji kushinda 1-0 ili wasonge mbele, baada ya kupata bao la ugenini lililofungwa na Thomas Ulimwengu Sudan, wakati Pirates wanatakiwa kulazimisha sare Misri.

No comments:

Post a Comment