Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, amemchambua kocha mpya msaidizi wa timu hiyo, Juma Mwambusi
na kumlinganisha na aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo, Charles
Boniface Mkwasa na kusema wawili hao hawana tofauti kabisa.
Mwambusi alichukua mikoba ya
Mkwasa ya kuwa msaidizi wa kocha, Hans Van Pluijm wiki iliyopita baada
ya Mkwasa kupewa mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuinoa timu ya taifa
ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Cannavaro alisema kuwa katika
kipindi alichokaa na Mwambusi amegundua kuwa kocha huyu hapendi utani
kwenye suala zima la nidhamu za wachezaji na siku zote amekuwa
akisisitizia suala hilo kama ilivyokuwa kwa Mkwasa.
Cannavaro alisema kuwa kutokana
na hali hiyo, hivi sasa ana matumaini makubwa sana na timu yao na
nidhamu haitakuwa tatizo kwenye kikosi cha Yanga kitu ambacho
kitachangia kuwapa ubingwa mapema msimu huu.
“Kwa muda mfupi niliokuwa na
Mwambusi baada ya kurejea kutoka Stars nimeona anaweka mbele masuala ya
nidhamu na kujituma kuliko kitu chochote na hivi ndivyo alivyokuwa
Mkwasa,” alisema Mwambusi.
“Mwambusi ni mtu wa utani sana na
tabia yake hii imesababisha wachezaji tumzoee haraka sana na tunaona
kama tumekaa naye zaidi ya mwaka, kinachonifurahisha zaidi ni kuwa
anapita kwenye njia zile zile za Mkwasa, hii itatusaidia kutupa matokeo
bora na inafahamika kuwa ili timu iwe bora lazima nidhamu izingatiwe,”
Cannavaro aliiambia Bingwa.
Cannavaro aliwataka pia wachezaji
wa kikosi hicho kufanya kazi kiweledi, kujituma na kufuata kila
wanaloelekezwa na benchi la ufundi kwani bado wana safari ndefu yenye
changamoto kuelekea katika kutetea ubingwa wao.
No comments:
Post a Comment