Wenyekiti
wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe ameamua kufunguka juu
ya mchezaji raia wa Senegal, Pape Abdoulaye N’daw ambaye amekuwa na
vituko katika siku za hivi karibuni, miongoni mwa matukio yake ya
kukumbukwa ni pamoja na kuingia uwanjani akiwa amevaa viatu vibovu
wakati Simba ilipocheza na Yanga.
Lakini kimbwanga kingine ilikuwa
ni kutuhumiwa kuwa na hirizi kwenye mechi iliyopita wakati Simba
ilipolala kwa goli 1-0 mbele ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa
Sokoine, jijini Mbeya.
“Unajua wachezaji wengi wanakuwa
na vituko mbalimbali lakini pia waandishi wa habari sasahivi naona
wamekuwa wanaropoka-ropoka sana kwasababu huyo N’daw hakuwa na hirizi
yoyote ila alikuwa amevaa ‘vest’ flan ndani ambayo ni nyeusi”, amesema
Poppe.
“Alikwenda kukaguliwa na kamisaa
na akarudi uwanjani, sasa watu wanaandika kwenye magazeti bila hata kuwa
na uhakika hata kusubiri ripoti ya kaimisaa na mwamuzi inasemaje.
Hakuwa na hirizi, alikuwa amevaa tu nguo tofauti kidogo na wachezaji wa
Prisons walikuwa wanafikiria anahirizi”.
“Unajua kwenye mpira wanasema
usivae kitu ambacho kitakuwa hatarishi kwa wenzio, na hakuwa na kitu
chochote zaidi ya nguo ya kawaida”.
No comments:
Post a Comment