9. Hristo Stoichkov: Mchezaji wa zamani wa Barcelona
“Van Gaal huwafanya wachezaji
wateseke, ukiangalia yeye mwenyewe alikuwa mchezaji wa kawaida sana,”
alisema mchezaji huyo wa zamani wa Bulgaria. “Anaharibu wachezaji wote,
kwa sababu ni mtu wa kawaida, angalia vizuri wachezaji ambao wameondoka
kwa sababu yake. Kwanza kabisa aliiharibu Barcelona kwa kipindi hicho,
na ikachukua muda mrefu mno kuijenga upya.”
8. Rivaldo: Mchezaji wa zamani wa Barcelona
“Van Gaal ni sababu kubwa ya kuondoka kwangu. Simpendi kabisa van Gaal, na nina uhakika kwamba hanipendi pia,” alisema Rivaldo.
7. Giovanni: Mchezaji wa zamani wa Barcelona.
“Van Gaal ni Hitler wa
wachezaji wa Kibrazil,” alisema Giovanni. “Ana majivuno, anaringa sana
yaani, kifupi ana matatizo sana. Maisha kati yangu na yeye yalikuwa ni
magumu na mabaya sana, Wabrazil hawamtaki kabisa, amenifanya nishuke
kiwango lakini vilevile aligombana na Rivaldo pamoja na Sonny Anderson.
“Mara zote alikuwa akituambia
hatukuwa tukifuata maelekezo yake vizuri mazoezini. Najua inawezekana
hana mawazo ya kisoka, hajui chochote, kwa kipindi chote nilichokuwa
naye nilikuwa nikifanya mazoezi ya aina moja tu, ni kama mgonjwa ama
chizi vile.”
6. Lucio: Mchezaji wa zamani wa Bayern Munich
“Ni ukweli usiofichika kwamba
kila kocha ana falsafa zake. Lakini hata hivyo, Van Gaal kwa kifupi
hakuwa na heshima kwangu. Nilistahili kuwa na heshima zaidi ya aliyokuwa
akinipa.”
“Van Gaal alinipa maumivu zaidi
ya mtu yeyote katika ulimwengu wa soka. Hakuwa hata akiongea nami kabla
ya baadaye kusema kwamba sikuwa nahitajika tena klabuni pale.
Inahuzunisha sana kwa kweli. Nilikuwa na wakati mzuri sana pale Bayern
na tulishinda makombe ya kutosha tu. Haikuishia hapo tu. Nilishinda
kombe la Shirikisho mara mbili, kombe la dunia nikiwa na Brazil na
kutangazwa kuwa beki bora wa ligi ya Bundesliga. Mimi sio kijana ambaye
natakiwa kuthibitisha thamani yangu kwa kocha mpya.”
5. Rafael Da Silva: Mchezaji wa zamani wa Manchester United.
“Najua hakuwa akinipenda, inawezekana sababu ni mimi kuwa Mbrazil, labda kweli ila sina uhakika na hilo.
“Najua historia yake kuwa huwa hapendi wachezaji wa Kibrazil, lakini siwezi kusema‘Oh, hapendi Wabrazil’
“Kiukweli sijui kwa sababu tangu Anderson aondoke, nilibaki mimi pekee ambaye ndiye nilikuwa Mrazil.”
4. Angel Di Maria: Mchezaji wa zamani wa Manchester United.
“Van Gaal ana falsafa zake na
moja ya vitu vilivyonifanya mimi kuondoka ni kwamba,”Di Maria alisema.
“Ni vigumu mno kuendana na Van Gaal. Nilikuwa na migongano mingi sana na
yeye.
“Nilianza vizuri sana pale
Manchester United lakini pale tu milipopata majeraha, mambo yakaanza
kwenda mrama na ndipo Van Gaal alipoanza kunichezesha nafasi tofauti. Na
nilipozungumza na (Laurent) Blanc akaniambia kuwa angenichezesha katika
nafasi ile ile niliyokuwa nikicheza Madrid endapo nitajiunga na PSG.”
3. Luca Toni: Mchezaji wa zamani wa Bayern Munich.
“Kifupi ni kwamba Van Gaal
hakutaka kufanya kazi na mimi, anawafanya wachezaji kama vitu
visivyobadilika,” alisema Toni. “Kocha alituhakikishia kuwa anaweza
kumwacha mchezaji yeyote. Aliamua kufanya kwa vitendo lakini kwa njia ya
kifasihi kwa kuvua suruali yake. Sikuwahi kukutana na kitu kama hicho,
yaani ilkuwa ni kitu cha ajabu kabisa. Lakini bahati nzuri sikuwa
nimeona chochote, kwa sababu sikuwa mstari wa mbele kama wenzanu
wengine.”
2. Frank Ribery: Mchezaji wa Bayern Munich
1. Zlatan Ibrahimovic: Mchezaji wa zamani Ajax Amsterdam.
‘Alikuwa ni kama dikteta.’
No comments:
Post a Comment