Saturday, October 3, 2015

Kiiza bado si shwari Simba


MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA Oktoba 3, 2015
Mgambo Shooting Vs Coastal 
Majimaji FC Vs Mwadui FC
Toto Africans Vs JKT Ruvu
Stand United Vs Mbeya City
Kagera Sugar Vs Prisons Kaitaba
Oktoba 17, 2015
Yanga SC Vs Azam Fc
Majimaji FC Vs African Sports
Mbeya City Vs Simba Sc Sokoine
Ndanda FC Vs Toto Africans
Stand United Vs Prisons
Coastal Union Vs Mtibwa Sugar
Mgambo Shooting Vs Kagera Sugar 
Mwadui FC Vs JKT Ruvu

SIMBA SC leo inatarajiwa kujua itamkosa kwa muda gani, mshambuliaji wake tegemeo la mabao, Mganda Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’.
Kiiza aliumia mazoezini mapema wiki hii, Simba SC ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Stand United juzi, wakishinda 1-0, bao pekee la Joseph Kimwaga.
“Majibu yake (Kiiza) tutayapata Ijumaa na ndiyo tutajua anahitaji kupumzika kwa muda gani,”amesema Gembe, ambaye awali alikuwa Daktari wa timu nyingine ya Ligi Kuu, Mtibwa Sugar.
Kiiza aliyueumia nyama za paja, hadi sasa ndiye kinara wa mabao wa Simba SC katika Ligi Kuu akiwa amefunga mabao matano katika mechi nne alizocheza.
Baada ya kupoteza mchezo mmoja tu katika mechi tano, nyingine zote ikishinda, Simba SC itarudi kwenye Ligi Kuu Oktoba 17, itakapomenyana na Mbeya City mjini Mbeya.
Lakini Ligi Kuu itaendelea kesho bila kuzihusisha Azam FC, Simba na Yanga SC, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Mgambo Shooting wakimenyana na  Coastal Union, Uwanja wa Majimaji, Songea wenyeji Majimaji FC wakiwakaribsiha Mwadui FC, Uwanja wa CC,m Kirumba,  Toto Africans wakiikaribisha  JKT Ruvu, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga Stand United wakiikaribisha Mbeya City na Uwanja wa A.H. Mwinyi, Tabora, Kagera Sugar wakiikaribisha Prisons.

No comments:

Post a Comment