Kiungo mjerumani Bastian
Schweinsteiger ameongeza idadi ya majeruhi kwenye klabu ya Manchester
United hivi sasa baada ya kuumia jana mazoezini akiwa na timu yake ya
taifa.
Nahodha huyo wa ujerumani, (31)
alishindwa kuiwakilisha timu yake ya taifa katika mchezo wa makundi wa
kufuzu kucheza fainali za mataifa ya ulaya EURO 2016 baada ya kuumia
ankle dakika chache akijiandaa na mazoezi.
Bastian anaungana na nahodha wa
Manchester United na England, Wayne Rooney ambaye naye atakosa michezo
miwili itakayochezwa na England leo Ijumaa na wiki ijayo kwa kuwa
majeruhi.
United pia iko katika hali mbaya
baada ya mlinzi wake muargentina Marcos Rojo naye kutokua fit kucheza na
hatimaye akaenguliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina.
Bado haijafahamika kama wachezaji
hao watakua fit tayari kuiwakilisha United katika mchezo mgumu dhidi ya
Everton weekend ijayo ya tarehe 17 October.
No comments:
Post a Comment