Kila kitu kinaenda vizuri kwa Kocha Juma
Mwambusi kutua Yanga kumsaidia Hans van Der Pluijm kuifundisha timu hiyo
akichukua nafasi ya Charles Mkwasa aliyepata kazi Taifa Stars.
Yanga hadi sasa ina orodha ya makocha kadhaa
waliotajwa kumudu kazi iliyokuwa ikifanywa na Mkwasa, lakini taarifa zinasema
Mwambusi anayeinoa Mbeya City ndiye mwenye nafasi kubwa ya kupewa dili hilo.
Mwambusi mwenyewe amekuwa mgumu wa kutoa
ufafanuzi kuhusu kuhusishwa kwake na Yanga kwani mara kadhaa hapokei simu yake
ikidaiwa yupo katika mazungumzo ya kina na viongozi wake.
No comments:
Post a Comment