Saturday, October 3, 2015

Siku za Blatter zahesabika, wadhamini wa kombe la dunia washinikiza aondoke

Utawala ndani wa Sepp Blatter ndani ya shirikisho la soka ulimwenguni unazidi kuandamwa na shinikizo la kumtaka aachie madaraka.
 
Baada ya wadau tofauti na viongozi mbalimbali kumshinikiza, leo hii kampuni ya Coca-Cola imekuwa mdhamini wa kwanza wa FIFA kumtaka Sepp Blatter aachie madaraka ya uraisi kwenye shirikisho hilo.
  Hatua hiyo ya CocaCola imekuja wiki moja baada ya Blatter kuanza kuchunguzwa rasmi a mamlaka za usalama za Uswisi kwa makosa ya kisheria yanayohusiana na fedha ndani ya FIFA, taasisi ambayo ameiongoza tangu 1998.
Blatter mwenye umri wa miaka 79 aliwaambia wafanyakazi FIFA kwamba amedhamiria kuendelea kuwa Raisi wa chombo hicho mpaka February mwakani utakapoitishwa uchaguzi wa dharula, lakini shinikizo jipya kutoka kwa wadhamini linaweza kumlazimu kujiuzulu.
 
“Kwa manufaa ya mchezo, kampuni ya Coca-Cola inamtaka Raisi wa FIFA kujiuzulu haraka ili ufanyike uchaguzi utakaorudisha heshima iliyopotea ya chombo hicho,” Coca-Cola ilisema kwenye taarifa yake.
“Kila siku inayopita, taswira na heshima ya FIFA inazidi kuharibika. FIFA inahitaji kusafishwa na hilo linaweza kufanyika kwa kuondoka waliosababisha hali hiyo.

No comments:

Post a Comment