Wiki hii kwa mara nyingine tena, Arsenal ilionekana kupata taabu
kuhimili mikimikiki ya soka la ulaya. Vipigo viwili mfululizo kwenye
michuano hiyo vimewaweka kwenye matatizo makubwa. Nafasi yao ya kushika
uongozi kwenye kundi lao ilikuwa tayari ngumu lakini sasa haionekani
hata kama watafanikiaa kufuzu.
Arsenal wamekuwa na rekodi mbaya katika michuano ya ulaya kwa muda sasa.
Katika msimu mitano iliyopita wametolewa kwenye raundi ya 16.
Tangu
walipomaliza wakiwa wa washindi wa pili msimu wa 2005/06, wamefika nusu
fainali mara moja, robo fainali mara mbili na mara zote zilizobaki
waliishia raundi ya 16. Hii ni rekodi ya kikosi cha hadhi ya kati, sio
klabu kubwa barani ulaya. Ni vigumu kuiita Arsenal klabu kubwa barani
ulaya wakati rekodi yao katika michuano mikubwa ya ulaya imekuwa ya
kuchechemea chini ya uongozi wa Wenger.
Hata
katika msimu wa 05/06 ilikuwa wazi kwamba haikuwa rahisi kwa wao kutwaa
uchampion na kwenye fainali wakiwa -0 uwanjani walifungwa na kikosi
bora cha FC Barcelona. Rekodi za Arsenal barani ulaya zinaonesha namna
Wenger alivyoshindwa kupambana na vigogo wengine barani humo. Pamoja na
kusifiaa nchini England, rekodi zake za ulaya zinaonesha uwezo wake wa
kuongoza na kuifundisha Gunners umeshindwa kumudu soka la ulaya.
Labda Wenger sasa ameifikisha Arsenal mahala ambapo inabidi ampe
kijiti mwalimu mwingine, kufeli kushindwa kubeba taji lolote kubwa tangu
kikosi chake kilipotwaa EPL bila kufungwa msimu wa 2003/04, Arsenal
imekwama. Makombe mawili ya FA Cup bado hayakidhi haja bila uwepo wa
taji la EPL au lolote la ulaya.
Arsenal,
katika ardhi yanyumbani bado hawaonekani kama wataupata ubingwa hivi
karibuni. Wenger ameunda kikosi chenye wachezaji wanaolipwa fedha nyingi
sana – usajili wa fedha nyingi wa Alexis Sanchez na Mesut Ozili
haujaimarisha timu ipasavyo. Timu inakosa wachezaji wanatakaoleta tija
kwenye maeneo yenye udhaifu ambao kwa miaka zaidi ya mitano umeendelea
kuwa tatizo kwenye timu. – hasa katika nafasi ya kiungo na ulinzi.
Lakini udhaifu huu bado haujashughulikiwa inavyopaswa. Je Wenger bado ni
mtu sahihi amwa kuipeleka Arsenal hatua nyingine au ndio ameshindwa
kabisa kukubaliana na ushindani mpya wa Chelsea na Manchester City.
No comments:
Post a Comment