Arsenal na Chelsea zinatarajia kushuka dimbani jumapili hii kuvaana katika mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu England maarufu kama EPL.Katika mchezo huo, mapato yote yatokanayo na mechi hutumika katika kuwasaidia watoto wa mtaani wasio jiweza na yatima.
Wachezaji wawili wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Diego Costa na Gary Cahil wote wana nafasi nusu ya kuivaa klabu ya Arsenal katika mchezo wa ufunguzi wa msimu nchini England kwenye mechi ya Ngao ya hisani jumapili hii.
Mlinzi Gary Cahil aliumia misuli ya pua alipofunga goli kuisawazishia timu yake ya Chelsea dhidi ya Barcelona katika mchezo uliomalizika kwa goli 2-2 na kisha Chelsea kushinda kwa mikwaju ya penati.
Akisisitiza hilo, kocha wa Chelsea Jose Mourinho anasema hajajua ukubwa wa tatizo la Cahil lakini akasema kuwa huenda akatakiwa kuvaa kinyago ‘mask’ ili acheze mechi ya jumapili.
Kwa upande wa mshambuliaji Diego Costa ambaye alitonesha matatizo yake ya ‘hamstring’ alifanyiwa mabadiliko ndani ya saa moja katika mchezo huo wa kimataifa dhidi ya Barcelona.
Kocha Jose Mourinho anasema bado haijajulikana uwezekano wa ushiriki wa wachezaji hao katika mchezo wa jumapili.
No comments:
Post a Comment