Thursday, July 23, 2015

Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli ameambiwa kuwa hatima yake ipo mikononi mwake.



Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli ameambiwa kuwa hatima yake ipo mikononi mwake.
Mchezaji huyo mtukutu raia wa Italia kwa sasa hajasafiri na wenzake wa Liverpool katika ziara kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi baadae mwezi Agosti.
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amenukuliwa akisema hana uhakika iwapo ataendelea kuwa na Balotelli Liverpool moja kwa moja katika msimu huu.
Liverpool imefanya ziara ya kujiandaa na ligi katika nchi za Asia , Australia na Malyasia lakini Balotelli yeye hakuwepo.

No comments:

Post a Comment