Mfaransa mweusi, mwenye asili ya
Mauritania, ambaye alitukanwa kutokana na rangi yake ya mwili na
mashabiki wa timu ya Chelsea kwenye kituo cha treni mjini Paris mwezi
February, amesema kuwa anataka waliomtusi waletwe kutoka Uingereza ili
washtakiwe kwenye mahakama ya Ufaransa.
Mkanda wa video
ulioonyesha kundi la mashabiki wakimzuia Bwana Souleymane Sylla
kupanda treni huku wakipiga mayowe wakisema "sisi ni wabaguzi wa rangi
na hivyo ndivyo tunavyopenda''.
No comments:
Post a Comment