Thursday, July 30, 2015

AZAM YAZIMA NDOTO ZA YANGA KUIFIKIA SIMBA, YAING'OA YANGA KAGAME


Ndoto za Yanga kutinga nusu fainali ya michuano ya Kagame na kutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame kwa mara ya sita, zimeishia njiani.

Waliofanya kazi hiyo ya kuzima ndoto za Yanga kutaka kuifikia Simba iliyobeba mataji sita, ni Azam FC.
Azam FC imeng’oa Yanga kwa kuitwanga kwa mabao 5-4 yote yakiwa ni ya miwaju ya penalty.
Katika mechi hiyo kwenye Uwanjawa Taifa jijini Dar es Salaam, timu hizo zilimaliza dakika 90 kwa sare ya 0-0.

No comments:

Post a Comment