Thursday, July 23, 2015

Buhari: Marekani inawasaidia Boko Haram!


Rais Mahammadu Buhari na Rais Obama
Marekani "inawasaidia na kuchochea " kundi la wanamgambo wa kiislam wa Boko Haram kwa kukataa kutoa silaha kwa Nigeria, ni kauli ya rais wa Nigeria Mahammadu Buhari.
Sheria ya Marekani inazuia serikali kuuza silaha kwa nchi ambazo zinashindwa kushughulikia ipasavyo masuala ya haki za binadamu.
 Wanawake nchini Nigeria
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alikutana na rais Barack Obama Jumatatu kuomba msaada zaidi.
Boko Haram limewauwa watu 10,000 tangu mwaka 2009 na limewateka mamia ya wasichana na wanawake.

No comments:

Post a Comment