Leo imeingia siku ya pili kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam
kujiandikisha katika daftari la kupiga kura kwa kutumia mfumo wa
kieletroniki maarufu kama BVR.
Katika zoezi hili ambalo linatarajiwa kudumu kwa siku kumi, tume ya
uchaguzi ya taifa inatarajia kusajili wakazi wapatao milioni tano ambao
wana sifa ya kupiga kura.
Hata hivyo, wakati zoezi hilo likiendelea, tayari linaonekana kuwa kero miongoni mwa wakazi.
Katika baadhi ya vituo ambao inaarifiwa kuwepo kwa ucheleweshwaji
huku katika maeneo mengine kukiwa na mashine chache za uandikishaji.
Je umejiandikisha kupiga kura katika mfumo huo mpya wa kielektroniki?
Tusimulie yaliyokusibu
No comments:
Post a Comment