Mji muhimu wa mwisho uliokuwa
mikononi mwa kundi la Al Shabaab kusini magharibi mwa Somalia wa
Baardheere umechukuliwa tena na vikosi vya Muungano wa Afrika (AU)
-miaka 7 baada ya wapiganaji hao wenye itikadi kali kuingia kwa mara ya
kwanza katika mji huo .
Wakazi wa mji huo wamesema vikosi vya
Kenya na Somalia vikiwa na silaha nzito na usaidizi wa mashambulizi ya
anga viliuvamia mji huo , ambao wapiganaji wa Al Shabaab waliutoroka
usiku.
Vikosi vya AU nchini Somalia, na vile vya jeshi la Somalia,
vilifanikiwa kuuteka mji huo baada ya mashambulizi makali. Majeshi
kutoka Kenya, Somalia na Ethiopia yamekua yakiendesha harakati za
kuuteka mji wa Baadheere kwa siku chache zilizopita.
Kumekuwa na mapigano makali viungani mwa mji huo, lakini wanamgambo
wa Alshaabab walisalim amri na kuukimbia ,na hivyo kutoa fursa ya mji
huo kuchukuliwa bila mapigano .
Wakazi wanasema kamanda mmoja wa
Somali na vyombo vya habari vinavyounga mkono Al Shabaab wamethibitisha
kuchukuliwa kwa mji huo.
Harakati hizo za kuuteka mji wa Baadheere zimefanikiwa siku chache
kabla rais wa Marekani Barack Obama kufanya ziara Afrika mashariki
ambapo suala la usalama nchini Somalia litakuwa kwenye ajenda kuu za
ziara yake .
Kundi la Al shaabab lina uhusiano na mtandao wa
kigaidi wa Al-Qaeda linapigana dhidi ya serikali ya Somalia kwa ajili ya
udhibiti wa nchi hiyo.
Wiki iliyopita mashambulizi ya ndege
zisizokua na rubani (drone) zilizoshambulia ziliripotiwa kuwauwa
makamanda wa ngazi ya juu wa Al Shabaab.
No comments:
Post a Comment