Mchezaji wa Chile kwa mara ya kwanza ameshiriki mazoezi na club yake mpya Bayern Munich ambayo inashiriki ligi ya Bundesliga.Vidal amejiunga na club hii akitokea Juventus na gharama iliyotumika kumfikisha Bayern ni kiasi cha £28million.
Thursday, July 30, 2015
PICHA 6 ZA ARTURO VIDAL AKIWA MAZOEZI KWA MARA YA KWANZA NA BAYERN MUNICH
Mchezaji wa Chile kwa mara ya kwanza ameshiriki mazoezi na club yake mpya Bayern Munich ambayo inashiriki ligi ya Bundesliga.Vidal amejiunga na club hii akitokea Juventus na gharama iliyotumika kumfikisha Bayern ni kiasi cha £28million.
AZAM YAZIMA NDOTO ZA YANGA KUIFIKIA SIMBA, YAING'OA YANGA KAGAME
Ndoto
za Yanga kutinga nusu fainali ya michuano ya Kagame na kutwaa ubingwa wa Kombe
la Kagame kwa mara ya sita, zimeishia njiani.
Waliofanya
kazi hiyo ya kuzima ndoto za Yanga kutaka kuifikia Simba iliyobeba mataji sita,
ni Azam FC.
Azam
FC imeng’oa Yanga kwa kuitwanga kwa mabao 5-4 yote yakiwa ni ya miwaju ya penalty.
Katika
mechi hiyo kwenye Uwanjawa Taifa jijini Dar es Salaam, timu hizo zilimaliza
dakika 90 kwa sare ya 0-0.
NGASSA APATA KIBALI CHA KAZI SAUZI NA KUWAAMBIA YANGA; “MLIKOSEA KUMUWEKA BENCHI MSUVA”
HATIMAYE kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amepata kibali cha kuishi na kufanya kazi Afrika Kusini, lakini amesema Yanga SC ilikosea jana kutomchezesha Simon Msuva.
Ngassa alikuwepo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana wakati Yanga SC ikitolewa kwa penalti 5-3 na Azam FC katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Na makocha Mholanzi, Hans van der Pluijm na mzalendo, Charles Boniface Mkwasa hawakumtumia kabisa Mchezaji Bora na Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simon Msuva, aliyeshuhudia mchezo wote akiwa benchi.
Ngassa aliyewasili jana mchana kuja kuchukua kibali cha kuishi na kufanya kazi Afrika Kusini Ubalozi wa nchi hiyo mjini hapa amesema; “Yanga SC wamekosea kutompanga Msuva,”.
Mchezaji huyo mpya wa Free State Stars ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini amesema kwamba Msuva ni mchezaji mwenye kasi na uzoefu, ambaye kama angechezeshwa jana, angeisaidia Yanga.
“Sijui kwa sababu gani hakucheza, kama alikuwa mgonjwa sawa, lakini alikuwa mzima na wakamuacha benchi tu, basi walikosea,”alisema Ngassa ambaye anaondoka jioni ya leo kurejea Bethelehem yalipo makao makuu ya FS.
Ngassa amesema kweli Yanga imesajili wachezaji wapya wenye kasi, Deus Kaseke na Godfrey Mwashiuya, lakini wote hao kuna vitu wanazidiwa na Msuva, haswa uzoefu.
“Mwashiuya mzuri, lakini anahitaji muda zaidi ili kujifunza kutokana na makosa yake na kupata uzoefu. Kaseke pia mzuri, si mfungaji sana kama Msuva na ndiyo anaanza kukusanya uzoefu,”amesema mume wa Radhia ‘Nish’.
Lakini kwa ujumla, Ngassa akamwagia sifa kiungo wa Azam FC, Himid Mao Mkami, kwamba alifanya kazi nzuri ya kutibua mipango ya Yanga uwanjani jana.
“Himid yeye jana alikuwa mtu wa kuharibu tu, na yule Mugiraneza (Jean Baptiste) alikuwa anasaidia vizuri ulinzi. Na Azam, kama Yanga walikuwa wanatumia mawinga kushambulia. Lakini nilivutiwa sana na Farid Mussa. Peke yake angekuwa mpishi wa mabao matatu kama nafasi alizotengeneza zingetumiwa vizuri,”amesema Ngassa.
Pamoja na hayo, Ngassa amesema kwamba ushindi wa Azam FC jana haumaanishi Yanga SC ni mbovu, bali ilizidiwa maarifa ya kimchezo na bahati haikuwa yao.
“Yanga SC wajipange tu, waangalie walikosea wapi wafanye marekebisho, baada ya hapo waje kulipa kisasi kwenye mechi ya Ngao ya Jamii (watakutana tena na Azam). Huo ndiyo mpira,”amesema Ngassa.
WACHEZAJI HAWA WANAWEZA KUKOSA MECHI YA NGAO YA HISANI ARSENAL vs CHELSEA
Arsenal na Chelsea zinatarajia kushuka dimbani jumapili hii kuvaana katika mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu England maarufu kama EPL.Katika mchezo huo, mapato yote yatokanayo na mechi hutumika katika kuwasaidia watoto wa mtaani wasio jiweza na yatima.
Wachezaji wawili wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Diego Costa na Gary Cahil wote wana nafasi nusu ya kuivaa klabu ya Arsenal katika mchezo wa ufunguzi wa msimu nchini England kwenye mechi ya Ngao ya hisani jumapili hii.
Mlinzi Gary Cahil aliumia misuli ya pua alipofunga goli kuisawazishia timu yake ya Chelsea dhidi ya Barcelona katika mchezo uliomalizika kwa goli 2-2 na kisha Chelsea kushinda kwa mikwaju ya penati.
Akisisitiza hilo, kocha wa Chelsea Jose Mourinho anasema hajajua ukubwa wa tatizo la Cahil lakini akasema kuwa huenda akatakiwa kuvaa kinyago ‘mask’ ili acheze mechi ya jumapili.
Kwa upande wa mshambuliaji Diego Costa ambaye alitonesha matatizo yake ya ‘hamstring’ alifanyiwa mabadiliko ndani ya saa moja katika mchezo huo wa kimataifa dhidi ya Barcelona.
Kocha Jose Mourinho anasema bado haijajulikana uwezekano wa ushiriki wa wachezaji hao katika mchezo wa jumapili.
RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA CHUO KIKUU CHA NEWCASTLE, AUSTRALIA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na Mstahiki Meya wa
jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes kabla ya kuanza kwa msafara wa
kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria
(Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle
Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015
katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe.
Nuatali Nelmes na viongozi wa chuo wakipata maelezo kabla ya kuanza kwa
msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari
wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe
29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika msafara wa kwenda jukwaa kuu
kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws
honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans
chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo
hicho.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viogozi wa chuo jukwaa kuu wakisimama
wakati nyimbo za Taifa za Tanzania na Australia zikipigwa wakati wa
kuanza kwa sherehe za kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa
Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe
29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Wasanii
wa kabila la Wakakulang wakicheza ngoma za asili yao katika kunogesha
sherehe za kihistorua ambapo Rais Kikwete amekuwa ni Mkuu wa Nchi wa
kwanza kupokea digrii hiyo ya heshima kutoka katika Chuo hicho.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle
Mhe. Nuatali Nelmes na viongozi wa chuo kabla ya kuanza kwa msafara wa
kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria
(Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle
Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015
katika ukumbi wa chuo hicho.
PICHA NA IKULU.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans Chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Sehemu ya umati wa wanachuo na wageni waalikwaa waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Sehemu ya umati wa wanachuo na wageni waalikwaa waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle .
Sehemu ya Watanzania waishio nchini Australia wakipiga makofi wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Kikwete akimpongeza Bi. Bernadette Mathias ambaye kwa kushirikiana na mpiga piano mumewe Profesa Philip Mathias walitumbuiza kwa wimbo wa "Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote" kwa ufasaha na kusisimua waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle
Rais Kikwete na msafara wa wanachuo wakiondoka jukwaa kuu huku wakishangiliwa na waliohudhuria ikiwa ni pamoja na Mama Salma Kikwete na mwana wao Ali Kikwete na ujumbe wa Rais Kikwete kwenye msafara huo.
Mama Salma Kikwete akimpongeza mume wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Newcastle na mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Ujumbe alioongozana nao mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja mkewe Mama Salma kikwete, mwana wao Ali Kikwete na Watanzania waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja mkewe Mama Salma kikwete, mwana wao Ali Kikwete na Watanzania na Waganda waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada.
Rais Kikwete akipongezwa na raia wa Burundi waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada.
Thursday, July 23, 2015
Ziara ya Obama:Anga ya Kenya kufungwa
Shirika linalosimamia safari za
ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga ya Kenya itafungwa kwa
muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii ili kuruhusu ndege ya
rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege
wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa shirika hilo, agizo
hilo litatekelezwa katika viwanja vyote vya ndege nchini Kenya na kuwa
anga hiyo itafunguliwa muda tu pale ndege hiyo ya rais Obama itakapokuwa
imetua.
Shirika hilo limesema kuwa limeyaandikia mashirika yote
ya ndege na pia kampuni zote za usafiri kuhusiana na agizo hilo na kuwa
safari za ndege kadhaa zitacheleweshwa siku hiyo na pia siku ya jumapili
wakati rais Obama atakapokuwa akiondoka nchini Kenya kuelekea Ethiopia
kwa muda wa dakika arubaini.
Awali idara ya polisi nchini Kenya ilikuwa imetangaza kuwa anga yote
ya Kenya itafungwa kwa muda wa siku tatu kabla ya ziara hiyo lakini kwa
mujibu wa shirika la KCAA ndege zote zinazopaa chini ya futi elfu
ishirini hazitaruhusiwa kutua katika uwanja wa Jomo Kenyatta na uwanja
wa wilson mjini Nairobi kuanzia siku ya Ijumaa hadi siku ya jumatatu,
wakati wa kongamano la kimataifa ya ujasiriamali litakalofanyika mjini
Nairobi.
Agizo hilo sasa linamaanisha ndege zote ndogo ndogo
ambazo uhudumu kati ya Nairobi na Somalia na viwanja vingine vidogo
vidogo katika kanda ya Afrika Mashariki, havitaruhusiwa kutua Nairobi
hadi mkutano huo utakapomalizika.
Rais wa Marekani Barrack Obama
anatarajiwa mjini Nairobi siku ya Ijumaa usiku ambapo anatarajiwa kuwa
mwenyeji wa kongamano hilo la kibiashara kwa pamoja na mwenyeji wake
rais uhuru Kenyatta.
Wakati huo huo, idara ya polisi nchini Kenya imetangaza ratiba ya usafiri wakati wa mkutano huo wa kimataifa.
Barabara
kuu kati kati mwa mji mkuu wa Nairobi na zile zinazoelekea, katika
makao makuu ya umoja wa mataifa mjini Nairobi zitafungwa wakati wa
mkutano huo, na idara hiyo imetoa wito kwa Wakenya kujiepusha na
shughuli katikati mwa mji na maeneo ya mkutano huo kuanzia siku ya
ijumaa hadi siku ya jumapili.
Buhari: Marekani inawasaidia Boko Haram!
Marekani "inawasaidia na kuchochea "
kundi la wanamgambo wa kiislam wa Boko Haram kwa kukataa kutoa silaha
kwa Nigeria, ni kauli ya rais wa Nigeria Mahammadu Buhari.
Sheria ya Marekani inazuia serikali kuuza silaha kwa nchi ambazo zinashindwa kushughulikia ipasavyo masuala ya haki za binadamu.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alikutana na rais Barack Obama Jumatatu kuomba msaada zaidi.
Boko Haram limewauwa watu 10,000 tangu mwaka 2009 na limewateka mamia ya wasichana na wanawake.
Usajili wa kielektroniki Tanzania umeanza
Leo imeingia siku ya pili kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam
kujiandikisha katika daftari la kupiga kura kwa kutumia mfumo wa
kieletroniki maarufu kama BVR.
Katika zoezi hili ambalo linatarajiwa kudumu kwa siku kumi, tume ya
uchaguzi ya taifa inatarajia kusajili wakazi wapatao milioni tano ambao
wana sifa ya kupiga kura.
Hata hivyo, wakati zoezi hilo likiendelea, tayari linaonekana kuwa kero miongoni mwa wakazi.
Katika baadhi ya vituo ambao inaarifiwa kuwepo kwa ucheleweshwaji
huku katika maeneo mengine kukiwa na mashine chache za uandikishaji.
Je umejiandikisha kupiga kura katika mfumo huo mpya wa kielektroniki?
Tusimulie yaliyokusibu
AU yateka ngome ya mwisho ya Al shaabab
Mji muhimu wa mwisho uliokuwa
mikononi mwa kundi la Al Shabaab kusini magharibi mwa Somalia wa
Baardheere umechukuliwa tena na vikosi vya Muungano wa Afrika (AU)
-miaka 7 baada ya wapiganaji hao wenye itikadi kali kuingia kwa mara ya
kwanza katika mji huo .
Wakazi wa mji huo wamesema vikosi vya
Kenya na Somalia vikiwa na silaha nzito na usaidizi wa mashambulizi ya
anga viliuvamia mji huo , ambao wapiganaji wa Al Shabaab waliutoroka
usiku.
Vikosi vya AU nchini Somalia, na vile vya jeshi la Somalia,
vilifanikiwa kuuteka mji huo baada ya mashambulizi makali. Majeshi
kutoka Kenya, Somalia na Ethiopia yamekua yakiendesha harakati za
kuuteka mji wa Baadheere kwa siku chache zilizopita.
Kumekuwa na mapigano makali viungani mwa mji huo, lakini wanamgambo
wa Alshaabab walisalim amri na kuukimbia ,na hivyo kutoa fursa ya mji
huo kuchukuliwa bila mapigano .
Wakazi wanasema kamanda mmoja wa
Somali na vyombo vya habari vinavyounga mkono Al Shabaab wamethibitisha
kuchukuliwa kwa mji huo.
Harakati hizo za kuuteka mji wa Baadheere zimefanikiwa siku chache
kabla rais wa Marekani Barack Obama kufanya ziara Afrika mashariki
ambapo suala la usalama nchini Somalia litakuwa kwenye ajenda kuu za
ziara yake .
Kundi la Al shaabab lina uhusiano na mtandao wa
kigaidi wa Al-Qaeda linapigana dhidi ya serikali ya Somalia kwa ajili ya
udhibiti wa nchi hiyo.
Wiki iliyopita mashambulizi ya ndege
zisizokua na rubani (drone) zilizoshambulia ziliripotiwa kuwauwa
makamanda wa ngazi ya juu wa Al Shabaab.
Souleymane Sylla: Nilidhalilishwa!
Mfaransa mweusi, mwenye asili ya
Mauritania, ambaye alitukanwa kutokana na rangi yake ya mwili na
mashabiki wa timu ya Chelsea kwenye kituo cha treni mjini Paris mwezi
February, amesema kuwa anataka waliomtusi waletwe kutoka Uingereza ili
washtakiwe kwenye mahakama ya Ufaransa.
Mkanda wa video
ulioonyesha kundi la mashabiki wakimzuia Bwana Souleymane Sylla
kupanda treni huku wakipiga mayowe wakisema "sisi ni wabaguzi wa rangi
na hivyo ndivyo tunavyopenda''.
Benteke ahamia rasmi Liverpool
Timu ya livepool imekamilisha
kumsajili rasmi mshambuliaji mwenye asili ya Jamuhuri ya Kidemokrasia wa
kongo Christian Benteke kutoka Aston Villa kwa kitita paundi milion
32.5.
Benteke alikubali mkataba wa muda mrefu na kuwa mchezaji wa pili kununuliwa kwa gharama kubwa huko England.
Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji ameifunga magoli 49 katika mechi 101 alizocheza kwenye timu yake ya zamani ya Aston Villa.
MAZOEZI YA SIMBA ZANZIBA-UWANJA WA AMANI
Makocha wakibadilishana mawazo
Kocha akitoa maelekezo
Wakifanya mazoezi ya viungo
Wachezaji Wakiwajibika mazoezi Mazoezini
Wachezaji wakiskiliza kocha
Kocha akitoa maelekezo kwa wachezaji wake akiwa na seleaman matola.
Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli ameambiwa kuwa hatima yake ipo mikononi mwake.
Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli ameambiwa kuwa hatima yake ipo mikononi mwake.
Mchezaji
huyo mtukutu raia wa Italia kwa sasa hajasafiri na wenzake wa Liverpool
katika ziara kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi baadae mwezi
Agosti.
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amenukuliwa akisema
hana uhakika iwapo ataendelea kuwa na Balotelli Liverpool moja kwa moja
katika msimu huu.
Liverpool imefanya ziara ya kujiandaa na ligi katika nchi za Asia , Australia na Malyasia lakini Balotelli yeye hakuwepo.
Nufaisha biashara yako kwa kutangaza na Mwanasoka
Blogu hii inamilikiwa na Gazeti la mwanasoka ambalo hutoka kilasiku ya alhamisi na jumapili kwa habari za michezo na burudani. Usilikose Gazeti hili kwa bei ya shilingi mia tano (500) tuu. Pia Tunapokea matangazo kwa gharama nafuu sana,Gazeti letu la mwanasoka linasambaa nchi nzima na nchi jirani za africa.Nufaisha biashara yako kwa kutangaza na Mwanasoka linalosomwa na maelfu ya watu.
Kwa mawasiliano zaidi piga:- 0656166050 au 0766838223
au tutumie habari/Matukio yoyote kupitia mwanasoka@hotmail.com
mwanasokans@gmail.com
Bonyeza hapa kutembelea blogu
Subscribe to:
Posts (Atom)